Vita vya Aleppo vyafikia ukingoni | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Aleppo

Vita vya Aleppo vyafikia ukingoni

Majeshi ya Syria pamoja na washirika wake wako kwenye hatua za mwisho za kuurejesha mji wa Aleppo baada ya kusonga mbele kwa ghafla na kufanikiwa kuwarudisha nyuma waasi ukingoni mwa kusambaratika

Awali, taarifa zilieleza kuwa, jeshi hilo limefanikiwa kukamata asilimia 98 ya eneo la Mashariki mwa mji wa Aleppo, ambalo awali lilishikiliwa na waasi. 

Taarifa zilizotolewa na Kiongozi wa kundi la waangalizi la Uingereza lenye makao yake nchini Syria, Rami Abdel-Rahman, zinasema kwamba vikosi vya waasi, vinashikilia asilimia 3 ya eneo hilo la Mashariki mwa Aleppo linalozungukwa. "tunaona kumalizika kwa vita hivi vya kuikomboa Aleppo", Abdel ameliambia shirika la habari la DPA. Amesema maeneo yaliyosalia mikononi mwa waasi ni machache mno, na yanaweza kukombolewa muda wowote.

Vita vya Mashariki mwa Aleppo ni lazima vimalizike haraka. waasi hawana muda zaid. wanatakiwa kusalimu amri ama kufa, Leftenant Generali Zaid al-Saleh, kiongozi wa serikali kwenye tume ya usalama ya Aleppo, amewaambia waandishi wa habari. Waasi wamekimbia hasa baada ya kuupoteza mji wa Sheik Saeed.

Msemaji wa waasi amesema kwenye taarifa yake kwamba, wapiganaji wa upinzani wanarudi nyuma upande wa Mashariki mwa Aleppo ambako kuna mashambulizi makali ya vikosi vya serikali ambayo kwa upande mwingine yanawaweka maelfu ya raia katika hali ya wasiwasi, na kuiita hali hiyo kuwa ni ya kutisha.

Syrien Zivilisten verlassen den Osten von Aleppo (Getty Images/AFP/G. Ourfalian)

Maelfu ya raia wanaukimbia mji huo wa aleppo kwa kuhofia usalama wao kutokana na mshambulizi

Taarifa ya jeshi imekuja masaa machache baada ya vikosi vya Syria vinavyoungwa mkono na wapiganaji wa Kishia wanaotoka Lebanon, Iraq na Iran kuuchukua mji wa Sheik Saeed, ambao ni miongoni mwa miji jirani iliyopo Kusini mwa eneo linalokaliwa na waasi.

Jeshi hilo limesema, mashambulizi yaliyofanywa leo hii yamefanikisha kukamatwa kwa mji jirani wa al-Fardos, ulioko katika eneo la Kaskazini mwa Sheik Saeed. Kiongozi wa kundi la waangalizi la Uingereza lenye makao yake nchini Syria, Rami Abdurrahman amesema mji huo bado unakabiliwa na mashambulizi. Miongoni mwa raia kwenye eneo hilo Assad Mahdo amesema ni pigo kubwa kuuwawa kwa raia.

Rais Bashar al-Assad anayeungwa mkono na Urusi hivi sasa yupo karibu na kuuchukua kabisa mji wa Aleppo, ambao kabla ya vita ulikuwa maarufu nchini Syria na hiyo itakuwa zawadi yake kubwa baada ya vita vya takriban miaka sita. Wizara ya masuala ya usalam ya Urusi imesema tangu kuanza kwa mashambulizi katika mji wa Aleppo, zaidi ya waasi 2,200 wamesalimu amri na raia 100,000 wamekimbia mji huo uliokuwa ukishikiliwa na waasi.

Taarifa nyingine kutoka kundi la wafuatiliaji nchini humo zinasema kiasi ya raia 34, miongoni mwao wakiwa ni watoto wameuwawa kwenywe shambulizi la anga katika kijiji kinachokaliwa na waasi wa kundi la Dola la Kiislamu, IS kilichopo eneo la jangwa nchini Syria. Mashambulizi hayo yamefanywa kwenye mkoa wa Uqayribat, uliopo kilomita 90 Kaskazini Magharibi mwa mji wa zamani wa Palmyra, ambao umechukuliwa na waasi kutoka majeshi ya serikali siku ya jumapili(11.12.2016)

Mwandishi: Lilian Mtono.
Mhariri: Saumu Yusuf. 


 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com