Vikosi vya Poland kuondoka Iraq mwakani. | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vikosi vya Poland kuondoka Iraq mwakani.

Warsaw.

Waziri mkuu wa Poland Donald Tusk ametangaza kuwa anataka kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo walioko Iraq ifikapo Oktoba 2008. Tusk amewaambia waandishi wa habari kuwa serikali mpya ya nchi hiyo inatoa ombi kwa rais ili kurefusha kuwapo kwa vikosi hivyo vya jeshi hadi Oktoba 2008 ili kuiwezesha Poland kukamilisha ujumbe huo.

Tusk ameongeza kuwa atazuru Iraq kabla ya Chrismas ili kutangaza kumalizika kwa ujumbe wa Poland nchini Iraq. Tusk amesema kuwa anamatumaini kuwa rais Lech Kaczynski , ambaye chama chake kimeshindwa na kile cha Tusk katika uchaguzi wa mwezi Oktoba , hatazuwia kuongolewa kwa vikosi hivyo vya jeshi. Kura ya maoni inaonyesha kuwa asilimia 85 ya watu wa nchi hiyo wanapinga kuendelea kuviweka vikosi vya jeshi la Poland nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com