Urusi yasema uchaguzi wa Hungary hautaathiri vita Ukraine
13 Aprili 2026
Matangazo
Peskov amesema ushindi huo na vita nchini Ukraine ni masuala mawili tofauti.
Amesisitiza kujitolea kwa Urusi katika kudumisha mahusiano mazuri na Hungary.
Peskov pia amesema raia wa Hungary wamefanya chaguo lao linalokubaliwa na Urusi akiongeza kuwa wamesikia taarifa kuhusu nia ya kushiriki katika mazungumzo hatua ambayo ni ya manufaa kwa nchi hizo mbili.
Hata hivyo amesema wanasubiri kuona jinsi nchi hiyo itakavyoendeshwa chini ya uongozi huo mpya wa Magyar .
Mara kwa mara, Orbán alipinga ufadhili wa Umoja wa Ulaya kwa Ukrainena kuendelea kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin hata baada ya uvamizi kamili nchini Ukraine mnamo Februari 2022