1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yadai kuchukua udhibiti wa kijiji cha Ukraine

6 Mei 2024

Jeshi la Urusi limedai kuchukua udhibiti kamili wa kijiji cha Ukraine cha Ocheretyne kinachokutikana kwenye mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo wa Donetsk.

https://p.dw.com/p/4fWy4
Vita vya Ukraine I Kijiji cha Ocheretyne
Athari za mapigano kwenye kijiji cha Ocheretyne cha nchini Ukraine.Picha: Anatolii Stepanov/AFP

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kukamatwa kwa eneo hilo kunaongeza nafasi ya vikosi vyake kwenye mstari wa mbele wa vita.

Jeshi la Ukraine lilikwisharipoti hapo kabla kuhusu kuingia kwa wanajeshi wa Urusi kwenye kijiji hicho lakini bado halijatoa taarifa rasmi ya kupoteza udhibiti wake.

Wafuatiliaji wa vita vya Ukraine wamebashiri kwamba hivi sasa Urusi inalenga kusonga mbele kuelekea mji muhimu wa Chasiv Yar ulio jirani na kijiji hicho.

Moja wapo ya malengo ya Moscow ni kuukamata mkoa wote wa Donetsk ambao ilikwishaunyakua kwa mabavu lakini imeshindwa kupata udhibiti kamili.