1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Upinzani Uturuki washinda uchaguzi wa manispaa Istanbul

1 Aprili 2024

Rais Recep Erdogan amesema leo kuwa Uturuki imo kwenye kipindi cha "mabadiliko makubwa" baada ya upinzani unaopinga utawala wake wa miongo miwili kushinda uchaguzi wa manispaa mjini Istanbul na miji mingine mikubwa.

https://p.dw.com/p/4eJMM
Meya wa mjini Istanbul Ekrem Imamoglu
Meya wa mjini Istanbul Ekrem ImamogluPicha: Chris McGrath/Getty Images

Matokeo yanayokaribia kukamilika yanaonesha chama kikuu cha upinzani cha Republican People's, CHP, kimeshinda miji mikubwa na majimbo kwenye rasi ya Anatolia ambayo ilikuwa ngome za chama cha Erdogan, AKP.

Mji wa kibiashara wa Istanbul, mji mkuu, Ankara na miji mingine ya Adana, Bursa na Antalya ilikuwa miongoni mwa manispaa zilizochagua mameya wa chama cha upinzani CHP jana Jumapili.

Soma pia: Zelenskiy atua Uturuki kufanya mazungumzo na Erdogan

Matokeo hayo yametokea chini ya mwaka mmoja baada ya jaribio lililoshindwa la kumuondoa Erdogan kupitia kura ya urais.

Wadadisi wameyataja kuwa matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi kwa Erdogan tangu chama chake kiingie madarakani mwaka 2002 na kuhusisha matokeo hayo na mfumuko wa bei wa asilimia 67 na kushuka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo lira, katika mwaka uliyopita.