1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

UNRWA yasema Wapalestina milioni moja wakimbia Rafah

28 Mei 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limesema kuwa takribani watu milioni moja wameukimbia mji wa Rafah katika muda wa wiki tatu zilizopita.

https://p.dw.com/p/4gN0K
Gazastreifen | Zerstörung in Rafah
Picha: EYAD BABA/AFP

Shirika hilo limeeleza kuwa wakimbizi hao hawana sehemu salama ya kwenda katikati ya mashambulizi ya mabomu, ukosefu wa chakula na maji na hali mbaya ya kibinadamu.

UNRWA imeongeza kuwa kwa sasa inakabiliwa na wakati mgumu hata kutoa misaada ya kibinadamu.

Mji huo mdogo ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza umekuwa ukiwapa hifadhi zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia mashambulizi ya Israel.

Wapalestina wengi wamelalamika juu ya mazingira magumu wanayokabiliwa nayo kila sehemu wanapokwenda.