1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

UN yahitaji dola bilioni 1.2 kuwasaidia Wapalestina

3 Novemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na masuala ya dharura limesema kunahitajika dola bilioni 1.2 kukidhi mahitaji ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza na kwenye ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel.

https://p.dw.com/p/4YNuR
Baadhi ya maeneo ya Gaza yaliyoharibiwa kwa makombora ya Israel
Baadhi ya maeneo ya Gaza yaliyoharibiwa kwa makombora ya IsraelPicha: Bashar Thaleb/AFP

Hiki ni kiwango mara nne ya kile kilichoombwa mwezi Oktoba na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

Fedha hizo zitatumika kugharamia mahitaji ya chakula, maji, huduma za afya na malazi kwa Wapelestina.

Blinken : Israel haina haki tu bali pia wajibu wa kujilinda

Msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema hii leo huko mjini Geneva kuwa hali ni ya kukatisha tamaa eneo hilo na kwamba msaada huo utasaidia kukidhi mahitaji ya raia wapatao milioni 2.7 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Watu milioni 1.5 wa Gaza wamekuwa wakimbizi wa ndani tangu kuanza kwa mzozo kati ya Israel na Hamas.