EU, Armenia wakubaliana kuimarisha ushirikiano
5 Mei 2026
Matangazo
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema makubaliano hayo yanaashiria hatua mpya ya ushirikiano kati ya pande hizo.
Ushirika wa Armenia na Urusi unasuasua
Armenia imekuwa na uhusiano wa mashaka na mshirika wake wa muda mrefu Urusi katika miaka ya hivi karibuni. Moja ya sababu ni walinda amani wa Urusi kushindwa kuingilia kati mizozo yake na Azerbeijan. Kwa upande wake Umoja wa Ulaya umeahidi kuiunga mkono Armenia, ukiitaja kama mshirika muhimu wa kibiashara.