Umeme hatimae warejea Gaza japo kwa mda | Habari za Ulimwengu | DW | 22.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umeme hatimae warejea Gaza japo kwa mda

GAZA:

Wakazi wa Gaza wamepata tena umeme japo kwa mda baada ya Israel kukubali kupelekwa mafuta katika mtambo pekee wa kuzalisha umemem wa Gaza.Israel ilikuwa imefunga mipaka yote na eneo la Gaza ambalo linadhibitiwa na kundi la Hamas kwa siku nne zilizopita.Hatua ya Israel yakufunga mipka yake na gaza ilisababisha onyo kutoka kwa Umoja waMataifa la kutokea mkasa wa kibinadamu.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani.Bi Condoleeza Rice akiwa mjini berlin kwa mazungumzo kuhusu mpango tatanishi wa nuklia wa Iran,amesema kuwa Marekani imezungumza na Israel kuhusu jinsi ya kuepusha mksa wa kibinadamu.

Hali ya wasiwasi ya baadhi ya WaPalestina ilidhihirishwa kwa njia moja katika mpka wa Gaza na Misri.Huko walinzi wa mpaka walitumia mabpmba ya maji na kufyatua risasi hewani ili kuwarejesha nyuma mamia ya wanawake waliojaribu kufungua kwa nguvu kivuko cha mpaka cha Rafah.

Hata hivyo wapalestina wenye silaha waliwafyatulia risasi walinzi wa mpka na kukafuatia mkanyagano wakati mamia ya wapalestina walipokuwa wanakimbia kufuatia milio ya risasi.Watu kadhaa

Mkiwemo watoto na wanawake wamejerihiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com