Ulaji rushwa nchini Tanzania
16 Oktoba 2007Matangazo
Miongoni mwa waliojitokeza kukosoa uongozi kwa kile wanachosema ni kushindwa kuwajibika katika vita dhidi ya rushwa ni aliyekuwa msaidizi wa rais wa kwanza wa taifa hilo hayati Mwalimu Julius Nyerere, Bw. Joseph Butiku. Akizungumza na Mohamed Abdulrahman kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam Bw. Butiku kwanza alikuwa na haya ya kueleza kwanini anafikiri rushwa imekithiri nchini humo.