Uholanzi yaanza kwa kishindo Euro 2008 | Michezo | DW | 10.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Uholanzi yaanza kwa kishindo Euro 2008

Italia jana usiku ilianza michuano kuwania taji la ubingwa wa soka barani Ulaya kwa kishindo, baada ya kuwachapa mabingwa wa dunia Italia mabao 3-0

Mlinda mlango wa Italia Gianluigi Buffon ambaye jana aliingia mara tatu nyuvuni kuokota mipira, katika kipigo cha mabao 3-0 walichopata

Mlinda mlango wa Italia Gianluigi Buffon ambaye jana aliingia mara tatu nyuvuni kuokota mipira, katika kipigo cha mabao 3-0 walichopata

Ulikuwa ni ushindi wa kusisimua kwa waholanzi, huku washabiki wengi kote duniani wakiduwaa kwani ni matokeo ambayo hayakutegemewa.


Ilikuwa ni shamra shamra na shangwe kote Uholanzi nchi yenye watu wenye wazimu wa mpira.


Vyombo vya habari nchini humo vimehanikizwa na habari za kuitukuza timu yao, ambapo gazeti la Volkskrant liliinadi habari hiyo kwa kichwa kisemacho Uholanzi yaanza michuano katika kundi la kifo kwa kiwango cha kusisimua.


Kundi C ambalo mbali ya Uholanzi na Italia pia lina na timu za Ufaransa na Romania ambazo hapo jana zilitoka sare ya bila kufungana.


Kundi hilo ndilo linaloaminika kuwa kuwa gumu kabisa kuliko makundi yote, yaani kundi la kifo.


Nalo gazeti la The Algemeen Dagblad limeandika Uholanzi yarejea kwa kishindo katika jukwaa la kimataifa.


Naye jogoo wa zamani wa Uholanzi, Johan Cruyff aliipongeza timu hiyo.Hapo kabla , Cruyff aliponda mbinu za kocha wa timu hiyo Marco van Basten.


Kwa upande mwengine Shirikisho la Soka Barani Ulaya limesema kuwa bao la kwanza la Uholanzi lililofungwa na Ruud van Nisterlrooy halikuwa na utata.


Hiyo ni kutokana na shutuma ya kwamba mfungaji aliotea kabla ya kupachika mpira huo wavuni.


Leo hii mabingwa watetezi Ugikiri wanaanza kamepni ya kutetea ubingwa wao kwa kuumana na Sweeden ambapo kabla ya hapo ya hapo Uurusi itapambana na Uhispania. • Tarehe 10.06.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EGv3
 • Tarehe 10.06.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EGv3