Uhispania mabingwa wapya dunia | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 12.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Uhispania mabingwa wapya dunia

Uhispania wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa kandanda wa dunia kwa mara ya kwanza huko nchini Afrika Kusini, baada ya kuifunga Uholanzi bao 1-0.

default

Mabingwa wapya wa dunia Uhispania na kombe lao

Bao hilo lilifungwa na Andreas Iniesta dakika chache kabla ya kumalizika kwa muda wa nyongeza, baada ya timu hizo kutoka suluhu katika muda wa kawaida. Uhispania pia ndiyo mabingwa wa Ulaya

Fußball-Nationalspieler Thomas Müller

Thomas Müller

Wakati huo huo mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller amekuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kutokana na mabao matano aliyofunga.Pia Muller ameteuliwa kuwa mchezaji bora kijana katika michuano hiyo.Diego Follan wa Uruguay alichaguliwa kuwa mwanasoka bora.

Kabla ya kuanza kwa pambano hilo la fainali kati ya Uholanzi na Uhispania, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliingia katika uwanja wa Soccer City akiwa kwenye gari la wazi ambapo alishangiliwa sana wakati alipozungushwa kuwasalimia watazamaji.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

 • Tarehe 12.07.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OGYM
 • Tarehe 12.07.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OGYM
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com