1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Tshisekedi na Kagame kusaini makubaliano ya amani Marekani

29 Novemba 2025

Marais wa Kongo na Rwanda watasafiri mjini Washington wiki ijayo kwa ajili ya kusaini makubaliano ya mwisho ya amani ili kumaliza vita mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/54Tv8
Angola Luanda | Treffen der Präsidenten Kagame (L)  Lourenco (C) und Tshisekedi
Marais wa Rwanda Paul Kagame(kushoto) Rais wa Angola Joao Lourenco (kati) na Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi Picha: JORGE NSIMBA/AFP

Marais wa Kongo na Rwanda watasafiri mjini Washington wiki ijayo kwa ajili ya kusaini makubaliano ya amani. Marais hao wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame wanatarajia kukutana pia na Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa utiaji saini makubaliano ya mwisho, yanayolenga kufikia amani ya kudumu katika eneo la mashariki mwa Kongo. Serikali ya Kongo imethibitisha juu ya hatua hiyo itakayohitimisha juhudi za kidiplomasia za miezi kadhaa zinazoongozwa na Rais Trump.

Rais Tshisekedi amethibithisha kwamba utiaji saini utafanyika Desemba 4, siku moja baada ya Rais Kagame kuonyesha matumaini kuhusu makubaliano hayo. Tshisekedi amesema amani ya kudumu katika eneo la mashariki mwa Kongo itaweza tu kupatikana ikiwa watu wanaohusika moja kwa moja watajitolea kufikia matokeo mazuri.