1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Trump/Netanyahu kujadili awamu ya pili ya mkataba wa amani

29 Desemba 2025

Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa hii leo kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwenye makazi yake binafsi ya Mar- a-Lago, Florida kujadiliana awamu inayofuata ya mpango wa amani wa Gaza.

https://p.dw.com/p/564WM
Israel Jerusalem 2025 | Donald Trump na Benjamin Netanyahu wakiwa kwenye Bunge la Israel, Knesset
Rais Donald Trump akizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika mkutano wa Knesset, Jumatatu, Oktoba 13, 2025, mjini Yerusalemu.Picha: Evan Vucci/REUTERS

Makubaliano hayo tete yenye vipengele 20 ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza yalifikiwa Oktoba 10 chini ya uratibu wa Washington yakiwa na lengo la kukomesha mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Hata hivyo, utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango huo ambapo Hamas watalazimika kusitisha mapigano na kutumwa kikosi cha kimataifa cha kutuliza hali unatarajiwa kuwa mgumu zaidi na hadi sasa Hamas inaipinga miito yote ya kupokonywa silaha.

Viongozi hao pia watajadiliana kuhusu Iran, ambayo Israel inaituhumu kuwa inaendelea kuongeza akiba yake ya makombora baada ya vita kati ya nchi hizo mbili mapema mwaka huu.