1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tinubu rais ajae wa Nigeria

Sudi Mnette
1 Machi 2023

Mgombea wa chama tawala nchini Nigeria Bola Tinubu ametangazwa kuwa mshindi wa katika kinyang'anyoro cha urais kinachozozaniwa, baada ya uchaguzi wa mwishoni mwa Juma.

https://p.dw.com/p/4O64J
Nigeria Wahl Bola Ahmed Tinubu
Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Tume ya Huru ya Uchaguzi au INEC kwa kifupi chake nchini Nigeria imeamtangaza Tinubu baada ya kuwapikua wapinzani wake wakubwa wawili. Anatajwa kufanikisha kupata asilimia 25 ya kura, ikiwa sawa na theluthi mbili ya majimba yote 36 ya Nigeria ukiwemo mji mkuu Abuja au la.

Shirika la habari la Uigereza-Reuters limefanya majumuisho kutoka kwa majimbo yote 36, miji mkuu ya majimbo na mji mkuu wa Abuja. Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) cha

Rais anayeondoka Muhammadu Buhari anatajwa kupta takriban asilimia 35 ya kura,au kura milioni 8.8, akifuatiwa na Atiku Abubakar mpinzani mkuu wa chama cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP), ambacho kilichukua asilimia 30 au kura milioni 6.9.

Mgombea kipenzi cha vijana Peter Obi wa Chama cha Labour, amepata asilimia 2 ya kura, au takriban  kura milioni 6.1.

Tinubu na matumani ya raia wa Nigeria.

Nigeria Wahl Bola Ahmed Tinubu
Rais mteule wa Nigeria Bola Ahmed TinubuPicha: Nengi Nelson/REUTERS

Kwa kukaa chonjo kwa Buhari, baada ya uchaguzi wa Jumamosi raia wengi wa Nigeria wana matumaaini kuwa kutafungua njia kwa kiongozi mpya kukabiliana na matatizo ya kiuchumi, usalama na kupunguza umasikini katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Chama cha upinzani cha PDP tayari kimeyaapuuzilia mbali matokeo ya uchaguzi huo na kudai uchaguzi mpya kutokana na kile wanachodai kuwa kuwekuwa na wizi mkubwa wa kura.

Tinubu mwenye umri wa miaka 70 ambae mwanasiasa wa muda mrefu nchini Nigeria, akiwa gavana wa jiji la Lagos 1999 hadi 2007 anatajwa kukabliwa na hoja za changamoto ya kiafya lakini pia kujinasua katika tuhuma za ufisadi katika miaka iliyopita, na ushirika wake wa Rais Buhari ambaye anatazamwa kama mtu aliyeshindwa kuifanya Nigeria kuwa salama.

Changamoto ya tume ya uchaguzi

Tume Huru ya Uchagzi nchini Nigeria (INEC) itoa ahadi ya kupakua matokeo kwa njia wa mtandao moja kwa moja kutoka kwa kila moja kituo cha kupigia kura kwenye tovuti yake lakini kwa sehemu kubwa ilishindwa kulitekeleza hilo na kiwango kikubwa cha matokeo hayo kikashindwa kuwekwa hadhari kwa njia hiyo.

Soma zaidi:Tinubu akaribia kupata ushindi wa uchaguzi nchini Nigeria

Kuna hofu ya yenye kuleta mvurugano kwa wengi kwamba mchakati huu wa uchaguzi na utoaji matokeo unaweza kuchagiza vurugu. Kwa mfano Jumanne hii katika soko la kawaida lenye shughuli nyingi kwenye jiji la kibishara la Lagos moja ya maeneo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, maduka mengi yalionekana kuwa yalifungwa na mitaa kuachwa wazi katika nyakati za asubuhi.

Vyanzo: RTR/AFP