1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu nne zinawania kuingia fainali kombe la dunia

Sekione Kitojo
9 Julai 2018

Timu nne zinawania  kuingia fainali  ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi Jumanne na Jumatano, wakati Ufaransa na Ubelgiji zitaoneshana kazi Jumanne, Uingereza na Croatia zina miadi siku ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/3164q
Fußball WM 2018 Russland - Kroatien
Picha: Reuters/H. Romero

Ufaransa  na  England  ni  vikosi  viwili vyenye wachezaji  vijana wenye umri mdogo zaidi  katika  kombe  la  dunia  na  vikosi  hivyo vinapambana   dhidi  ya  Ubelgiji  na  Croatia, timu zenye wachezaji wenye  uzoefu  zaidi,na umri mkubwa kidogo, katika  nusu  fainali  ya kombe  la  dunia  mwaka  huu.

Fußball WM 2018 Schweden - England
Chipukizi wa Uingereza mara hii wamefanya vizuri lakini je watashinda dhidi ya uzoefu wa Croatia ?Picha: Reuters/M. Rossi

Chipukizi ama  uzoefu  ni  swali  ambalo mara  nyingi  hujitokeza katika  kandanda  na  hususan  katika  michezo  hii  iliyoko  katika awamu  ya  mwisho ya  kombe  la  dunia  hakuna  tofauti.

Michezo  yote  ya  nusu  fainali  ina  timu  moja  yenye  makinda ikitarajia  kufanya  vizuri  na  vijana  wa  zamani  kwa  upande mwingine wako  upande  mwingine wakipambana  nao.

Kikosi  cha  Didier Deschamps cha  Ufaransa na  Gareth Southgate wa  England ni  vikosi  vya  pili kwa vijana  wadogo katika mashindano  haya, vikiwa  nyuma  tu  ya  Nigeria, kwa  wastani wa umri  wa  miaka  26.

Wakati  huo  huo timu  hizi zinakumbana  uso  kwa  uso  hapo  Julai 10  na  11, na  Ubelgiji  na  Croatia, ambazo  zina  wastani  wa  umri wa  miaka  27.6 na  27.9.

Tofauti  hii inachochewa  zaidi  wakati ukiangalia  vikosi  vilivyoanza katika  ushindi wao katika  robo  fainali.

Fußball WM 2018 Russland - Kroatien
Wachezaji wenye umri wa juu kidogo na uzoefu wa Croatia Luka Modric (8) Brozovic(11) Vida (21) na Rebic (18).Picha: Reuters/M. Shemetov

England ilifika nusu  fainali kwa  ushindi  bila  taabu  wa  mabao 2-0 dhidi  ya  Sweden na  kikosi  kilichoanza  kilikuwa  na  wastani  wa umri  wa  miaka 25.6. Ufaransa  ilikuwa  na  wastani  wa umri  wa miaka  25.1 na  kupita  dhidi  ya  Uruguay kwa  matokeo  kama hayo.

Dalili njema kwa Uingereza na  Ufaransa

Wakati  huo  huo kikosi  cha  Ubelgiji  kilichoanza  katika  ushindi  wa mabao 2-1  dhidi  ya  Brazil kilikuwa  na  wastani  wa  umri  wa miaka  28.2  na  Croatia  ilipoishinda  Urusi  kwa  mikwaju  ya  penalti kilikuwa  na  wastani  wa  umri  wa  miaka  29.2.

Kutokana  na  kwamba  Italia  mwaka  2006 ilikuwa  timu pekee kuweza  kushinda  kombe  la  dunia  ikiwa  na  kikosi kilichokuwa  na wastani  wa  umri  wa  miaka  28, kwa mujibu wa  gazeti  la Telegraph, huenda  ni  hali  bora  kwa  Uingereza  na  Ufaransa.

Fußball WM 2018 Brasilien - Belgien |  Romelu Lukaku
Mshambuliaji Romelu Lukaku akishangiria ushindi wa Ubelgiji dhidi ya BrazilPicha: picture-alliance/Sputnik/M. Bogodvid

Nae  rais  wa  Ufaransa Emmanuel Macron atahudhuria  pambano  la kesho  la   nusu  fainali  katika  kombe  la  dunia  kati  ya  ufaransa na  Ubelgiji mjini  St. Petersburg. Utaratibu  wa  shughuli  za  kila  siku za  rais  umethibitisha  jana  Jumapili  kwamba  Macron atashuhudia timu  yake ikipambana  kuwania  nafasi ya  kucheza  fainali ya kombe  la  dunia  siku  ya  Jumapili. Macron alisema  kabla  ya mashindano  haya  kwamba anaweza  kwenda  nchini  Urusi  iwapo les Bleus watafanikiwa  kufikia  nusu  fainali.

Kwa upande  mwingine  Croatia imefanikiwa  kufuata  nyayo za kikosi  cha  mwaka  1998 kwa  kufika  katika  nusu  fainali  ya kombe  la  dunia. Na kwa  kuwa  wana  Luka  Modric huenda wakapiga  hatua  moja  zaidi  katika  nusu  fainali dhidi  ya  England.

Kwa  mujibu wa  mchezaji mkongwe nyota  wa  Croatia  Davor Suker Luka  Modric anastahili kupata tuzo  ya  mpira wa  dhahabu  kwa kuwa  mchezaji  bora wa  mashindano  haya.

Galerie Fußball-WM-Torschützenkönige Davor Suker
Davor Suker wa Croatia mwaka 1998 alipoiongoza Croatia kufikia nusu fainali ya kombe la duniaPicha: Getty Images/AFP/Gerard Cerles

Modric mwenye  umri  wa  miaka  32 hakuwa  na  bahati katika mkwaju  wake  wa  penalti ambao uliokolewa  na  mlinda  mlango  wa Urusi  Igor Akinfeev. 

Lakini mchezaji  huyo  nyota  wa  Real Madrid anaweza  kuonesha  tofauti wakati  Vroatia  ikilenga  kuchukua hatua  moja  zaidio kuliko kikosi kilichokuwa  kinaongozwa  na  Suker cha  mwaka  1998 na  kufikia  fainali  ya  kombe  la  dunia  wakati watakapokutana  na  England  katika  nusu  fainali siku  ya Jumatano mjini  Moscow.

Russland WM 2018 Argentinien gegen Kroatien
Mchezaji wa kati wa Croatia na Real Madrid Luka ModricPicha: Reuters/I. Alvarado

Modric  binafsi  hasumbuliwi  na  kupata  taji  la  mpira  wa  dhahabu ama  tuzo ya  mchezaji  bora  wa  dunia  mwezi  Septemba kwasababu , "kitu muhimu  hivi  sasa  ni  Croatia."

"Tumekwisha fikia kitu fulani lakini  timu  hii inaweza  kufanya  zaidi," alisema Luka Modric.

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Khelef