Tanzania: Sababu za kurefushwa tume ya vurugu za uchaguzi
8 Aprili 2026
Ongezeko hilo la siku litaifanya ripoti kuwekwa hadharani Aprili 24 jambo ambalo limezua maswali na mjadala miongoni mwa watanzania ambao wengi macho na masikio yao yalikuwa yakisubiri ripoti hiyo.
Jaji Chande ambaye ni Mwenyekiti wa tume hiyo amezungumza na wanahabari Jumatano ikiwa ni siku moja baada ya gazeti la serikali kutangaza nyongeza ya muda wa uchunguzi wa tume hiyo kwa siku 21 na kutaja sababu ya ongeko hilo kuwa ni kuchambua kwa kina Ushahidi mwingi uliopatikana na kutengeneza tafsiri ya Kiingereza. Mengine ni haya aliyoyasema Jaji chande ni haya. "Ushahidi mwingi unaendelea kuja, pili ushauri wa kitaalumu ambao tumeuomba, na washauri wa kitaalamu wanatupa, tatu kuchambua kwa kina shahidi mwingi ambao tumeupata”
Novemba 18 mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan, aliunda tume ya watu wanane kuchunguza vurugu hizo zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu.
Aidha, Jaji Chande amesema kuwa awali walipanga kufanya uchunguzi katika mikoa sita lakini wamelazimika kufikia mikoa 12 na kukusanya taarifa mfano kwanini Arusha kuwe na ghasia kubwa alafu Kilimanjaro zisiwepo, au Zanzibar kuwe shwari lakini Dar es salaam kuwe na ghasia wakati maeneo hayo yapo karibu.
Akaongeza kuwa wanataka ripoti ikitoka iwasemee Waathirika na wajione wametendewa haki, na Tume hiyo imependekeza Maridhiano ili kurejesha mshikamano na umoja.
Hata hivyo baadhi ya wadau wa masuala ya haki za binadamu na utawala bora wamelalamikia muda mrefu wa kukamilika kwa ripoti hiyo ambayo Februari 22 iliongezewa siku 42.
Mwanaharakati wa haki za binadamu, Wakili Ana Henga amesema kuwa kucheleweshwa kwa ripoti hiyo niawa na kuminya haki za waathirika. "Ushahidi wa kisayansi sidhani kama unachukua muda wote huo siku 42 jumlisha siku 21, sidhani kama ni sababu za msingi anatoa, waniwie radhi kusema hivyo lakini watanzania tuna tatizo kubwa”
Msemaji Serikali, Gerson Msigwa amesema, uvumilivu ni jambo la busara ili tume hiyo ifanye kazi yake vyema ili hapo baadaye kusiwe na malalamiko yoyote. "Kwa upande wa serikali tungependa tume itakajapokuja na ripoti kusiwepo mtu atakayesema maoni yangu hayakuzingatiwa, tuiache tume ifanye kazi yake, hata wale wenye haraka ripoti hii itakuwa na maana kama ripori itakuwa bora”
Oktoba 29 wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania, ziliibuka vurugu zilizochagizwa na maandamano yaliyosababisha uvunjifu wa amani, mauaji na uharbifu wa mali, ndipo Rais Samia Suluhu aliopiunda tume huru kuchunguza vurugu hizo mwaka jana.