Tanzania kupeleka kikosi Dafur | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tanzania kupeleka kikosi Dafur

Tanzania itachangia wanajeshi 800 katika kikosi mchanganyiko cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuleta utulivu na kukomesha mauaji ya raia katika jimbo la Dafur nchini Sudan .

Waziri wa Ulinzi Juma Kapuya amesema wanajeshi wake watakaowekwa Dafur hapo mwezi wa Machi hawatohusika na mapambano wakati wakipiga doria katika jimbo hilo ambapo tayari wanajeshi wa kulinda amani wamekuwa wakishambuliwa na kuuwawa.

Kwa mujibu wa Kapuya wana baraka zote za serikali ya Sudan ambayo imeiomba Tanzania kuchangia kwenye kikosi cha kimataifa cha kulinda amani kuleta utulivu Dafur.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com