1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 518 waliuwawa katika ghasia za uchaguzi Tanzania

23 Aprili 2026

Tume ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania imebainisha kuwa watu 518 waliuwawa katika vurugu zilizotokea kipindi hicho.

https://p.dw.com/p/5CjOi
Tume ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania imetoa ripoti yake
Jaji Mohamed Chande OthmanPicha: Tanzania state House 

Ripoti iliyowasilishwa Alhamisi na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mohamed Chande Othman imesema zaidi ya watu 800 walijeruhiwa kwa risasi. Jaji Chande amesema idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi kwa sababu baadhi ya familia ziliwazika wapendwa wao bila kuwapeleka kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti.

Rais Samia kufanyia kazi mapendekezo ya tume

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan amejibu kuwa ameyapokea mapendekezo ya tume hiyo na atayafanyia kazi.

Tanzania ilikumbwa na ghasia hizo wakati wa uchaguzi baada ya vijana kuingia barabarani wakiishutumu serikali kwa kuunkandamiza upinzani. Tume hiyo imesema maandamano hayo hayakuwa ya amani, yaliratibiwa, na imetaka uchunguzi zaidi kuhusu matumizi ya silaha.