1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Sunak atangaza msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine

Sylvia Mwehozi
13 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ametangaza msaada mpya wa mabilioni ya dola kwa Ukraine, wakati alipofanya ziara ya kushutukiza mjini Kyiv jana Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4bBwu
Rishi Sunak mjini Kiev
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyyPicha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ametangaza msaada mpya wa mabilioni ya dola kwa Ukraine, wakati alipofanya ziara ya kushutukiza mjini Kyivjana Ijumaa.

Msaada huo unatolewa katika wakati muhimu kwa Ukraine huku washirika wake wa nchi za Magharibi wakipambana kutafuta ufadhili na Urusi nayo ikiimarisha hifadhi yake ya silaha na safu ya wanajeshi.

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amesifu makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama wa miaka 10 pamoja na msaada wa kijeshi wa paundi bilioni 2.5 uliotengwa kwa mwaka 2024.

Msaada huo unajumuisha aina mbalimbali za silaha na risasi ambazo ni adimu nchini Ukraine, kama vile makombora ya mizinga na ndege zisizo na rubani.

Ziara ya kiongozi huyo wa Uingereza imefanyika huku maafisa wa Ukraine wakisema kuwa shambulizi la makombora ya Urusi limewaua watu wawili katika mji wa Kherson kusini mwa nchi hiyo.