SPD chajipatia uongozi mpya | Magazetini | DW | 20.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

SPD chajipatia uongozi mpya

Steinmeier na Müntefering wawajibika kukiongoza chama cha SPD kuelekea ushindi wa uchaguzi mkuu mwakani.

default

Frank-Walter Steinmeier na Franz MünteferingKuteuliwa Steinmeier na Münterfering kuongoza chama cha Social Democratic kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani,mpango wa serikali wa kuunusuru uchumi,ikiwa ni pamoja na uamuzi wa Deutsche-Bank wa kutozigusa fedha zilizoahidiwa na serikali za kuunusuru uchumi-Hizo ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.


Kuhusu kuteuliwa uongozi mpya wa chama cha SPD ,gazeti la Die WELT limeandika:


Chama cha SPD kilizongwa na mizozo ya ndani kwa muda wa miezi kadhaa.Kuteuliwa mwenyekiti wa nane wa SPD,tangu mwaka 1991,ni ishara kwamba mambo hayakua bambam hivyo katika uongozi wa chama kikongwe kabisa cha kisiasa nchini Ujerumani. Dalili lakini zimeshaanza kuchomoza Steinmeier na Müntefering ndio muwafak.Wiki sita baada ya mkutano mkuu wa dharura wa SCHIELOWSEE,chama cha SPD kimeanza kuimarika.Kujiuzulu mwenyekiti aliyepotea njia Kurt Beck ,ilikua sawa na kukikomboa chama hicho.Kwa muda mrefu sasa wana Social Democratic hawajawahi kuonekana  wachangamfu kama walivyo hivi sasa.Msimu wa kiangazi wa mwaka 2008 umepelekea kuchipuka upya chama cha SPD.."


Hayo ni maoni ya Die WELT.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linahisi,Steinmeier na Müntefering wanalingana vizuri kabisa.Gazeti linaendelea kuandika:


Mgombea wadhifa wa kansela anaweza kumtegemea mwenyekiti wa chama,sawa na jinsi mwenyekiti wa chama anavyoweza kumtegemea mgombea kiti cha kansela.Sababu ziko chungu nzima:Kwanza wamekua wakishirikiana tangu mwaka 1998.Pili msimamo yao ya kisiasa inalingana ,hasa tangu Müntefering alipo jitambulisha mnamo mwaka 2003 na ajenda 2010.Tatu Müntefering hakutaka na wala hataki kuwa kansela.Nne tafsiri yao kuhusu uongozi wa kisiasa inafanana.Kwao wao uongozi manaake kutoa muongozo na kuutekeleza."


 Gazeti la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG linazungumzia hatua za kuinua shughuli za kiuchumi na kuendelea kuandika:


"Angalao habari za kutia moyo kwa waajiriwa,wastaafu na wanunuzi.Mpango wa serikali kuu umelengwa kuwapa motisha raia wanunue vitu.Zaidi ya hayo mpanho huo unaweza kuchangia kurejesha imani ya wananchi ambayo imefifia kutokana na mzozo wa fedha.Hata hivyo tusitegemee kwamba,kiu cha wanaunuzi kitakua kikubwa hivyo eti kwasababu serikali kuu ya muungano imeamua kuwapunguzia kodi za mapato.Fedha zitakazotokana na nafuu hizo si nyingi hivyo na hofu za wananchi bado hazijatoweka.


 • Tarehe 20.10.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FdSH
 • Tarehe 20.10.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FdSH
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com