1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Rais Kiir amteua 'marehemu' kwenye kamati ya uchaguzi

3 Februari 2026

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemteua bila kukusudia mtu aliyekufa kuwa mjumbe wa kamati itakayoandaa uchaguzi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/57zw8
Uganda Entebbe 2024 | Mkutano wa IGAD | Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwasili Uganda
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Msemaji wa ofisi ya rais Salva Kiir amesema hii leo kwamba mamlaka zilipitiwa wakati wa uteuzi baada ya Steward Sorobia Budia, mwanasiasa wa zamani wa upinzani kuwa miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika amri iliyotolewa na Kiir.

Budia alifariki miaka mitano iliyopita.

Taarifa zinasema familia ya marehemu sasa inadai fidia, kwa kuzingatia tamaduni zinazokataza kuomba au 'kuamsha' roho ya marehemu bila ufahamu, ridhaa au ushiriki wa familia.

Hakujawahi kufanyika uchaguzi nchini Sudan Kusini iliyopata uhuru tangu 2011, na ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kila mara.