Putin kuwa waziri mkuu.
18 Desemba 2007Matangazo
Moscow. Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kuwa atakubali kuwa waziri mkuu iwapo meneja wake wa zamani wa kampeni Dmitry Medvedev atashinda uchaguzi wa rais mwezi March mwakani. Putin amesema hayo katika mkutano mkuu wa chama cha United Russia mjini Moscow, ambako Medvedev ameteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tikiti ya chama hicho. Putin haruhusiwi kugombea mara ya tatu kiti cha urais kwa mujibu wa katiba ya Urusi, lakini kama waziri mkuu Putin atakuwa na wadhifa wa pili wenye nguvu katika siasa za Urusi. Ushindi kwa Medvedev ni hakika katika uchaguzi ujao.