1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pretoria yakaribisha ombi la mwendesha mashitaka wa ICC

Sylvia Mwehozi
21 Mei 2024

Afrika Kusini imekaribisha ombi la mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC la kutaka kukamatwa kwa viongozi wa Israel na Hamas.

https://p.dw.com/p/4g5AM
Cyril Ramaphosa| Rais wa Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: SIPHIWE SIBEKO/REUTERS

Afrika Kusini imekaribisha ombi la mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC la kutaka kukamatwa kwa viongozi wa Israel na Hamas. Taarifa ya ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema kuwa sheria lazima itumike kwa usawa ili kuzingatia utawala wa sheria wa kimataifa, kuhakikisha uwajibikaji kwa wale wanaofanya uhalifu wa kutisha na kulinda haki za waathiriwa.Mwendesha mashtaka ICC aomba waranti dhidi ya Netanyahu, viongozi wa Hamas

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Afrika Kusini inajitolea katika utawala wa sheria ya kimataifa, kuheshimu haki za binadamu kwa wote na kusuluhisha mizozo yote ya kimataifa kwa njia ya mazungumzo na sio vita, na kujitawala kwa watu wote, ikiwa ni pamoja na Wapalestina.

Hapo jana mwendesha mashitaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya ICC Karim Khan, alisema kuwa ameomba waranti ya kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant na viongozi watatu wa kundi la wanamgambo la Hamas kufuatia madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita.