Papa akutana na wahanga wa unyanyasaji wa kingono
20 Oktoba 2025
Tim Law, muanzilishi mwenza wa taasisi ya Ending Clergy Abuse (ECA), iliyoko Marekani iliyo na lengo la kusitisha unyanyasaji unaodaiwa kufanywa na makasisi amesema, nia hasa ya mkutano huo ni kuwa na uhusiano mwema na Papa Leo na kupata hakikisho lake la kujadili masuala haya kwa uwazi. Amesema Papa ameridhia matakwa yao.
Tim ameongeza kuwa mkutano huo uliowahusisha pia mawakili wanaowawakilisha wahanga haokutoka zaidi ya mataifa 30 ulipaswa kufanyika kwa dakika 20 tu lakini ulirefushwa hadi saa moja.
Kundi hilo limemtaka Papa Leo kuweka sheria ya kutovumilia unyanyasaji na kukomesha kabisa dhuluma hiyo. Amesema tayari sheria hiyo inafanya kazi nchini Marekani kwa makanisa yote. makanisani. ambayo tayari imewekwa nchini Marekani kwa
Chini ya sheria iliyoundwa na maaskofu wa Marekani, kasisi anapaswa kuondolewa kikamilifu kutoka katika huduma za kikanisa iwapo kisa chochote cha unyanyasaji wa kingono wa watoto chini ya miaka 18 kitakachothibitishwa dhidi yake.
Wahanga hao wamesema hayo, siku chache tu baada ya Tume ya Vatican ya kuwalinda Watoto kuwashutumu viongozi wa ngazi ya juu kanisani humo kusuasua katika suala zima la kuwasaidia wahanga.Kwa miongo mingi, kanisa Katoliki limekuwa likitikiswa na kadhia ya kuficha uovu huo, hali ambayo inachafua jina na sifa ya kanisa mbali na hasara ya mamilioni ya dola kulipa fidia.
Mwezi Mei ECA awali ilikuwa imemuandikia barua Papa Leo XIV,ikiomba kukutana na kiongozi huyo wa kiroho baada ya kuchaguliwa kama kiongozi wa waumini takriban bilioni 1.4 duniani.
Vatican ilithibitisha Papa Leo kukutana na wajumbe wa ECA , lakini haikutoa taarifa zaidi ya kile kilichozungumzwa.