1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Odinga apata viti vingi vya ugavana Nairobi

10 Agosti 2022

matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yanaonesha muungano wa azimio ambao unaongozwa na Raila Odinga umeafikiwa kupata viti vingi katika jimbo la Nairobi.

https://p.dw.com/p/4FNPe
Kenia Wahlen 2022, Raila Odinga
Picha: Tony Karumba/AFP

Pamoja na hatua hiyo kwa upande mwingine muungano wa Kenya Kwanza wa William Ruto ukijinyakulia kiti cha ugavama baada ya zoezi la kupiga kura la Jumanne. Matokeo hayo yametangazwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Kenya.

Wakazi wa Jimbo la Nairobi ambalo ndilo jiji kuu taifa la Kenya, kwa mara nyingine tena wameonesha upendo wao kwa kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga kwa kuwapa wajumbe wa muungano huo nafasi ya kuwaakilisha kwenye bunge la taifa.

Odinga kupata nyongeza ya nguvu.

Hatua hiyo inamuongezea nguvu Raila ambaye anawania kiti cha urais huku matokeo ya hivi punde yakionyesha kuwa anakabana koo na mpizani wake wa karibu William Ruto wa Kenya Kwanza.  Hata hivyo jimbo hili dogo kati ya majimbo 47 nchini Kenya lina maeneo bunge 17 ambayo kihistoria yamekuwa yakiwakilishwa na chama cha ODM cha Raila.

Kulingana na matokeo ya awali ya tume ya kusimamia uchaguzi hali hiyo itasalia hivyo. Hayo yanajiri baada ya mjumbe wa Langata Nixon Korir kukubali kushindwa hata kabla ya IEBC kutangaza mshindi. Kiti hicho kimetwaliwa na mgombea wa Azimo Nixon Odiwor aliyekuwa mwanahabari.

Mbunge wa Makadara George Aladwa kwa tikiti ya Azimio amekihifadhi kiti hicho baada ya wagombea wa vyama tanzu vya Azimio kumuunga mkono kwenye kinyang'anyiro hicho.

Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi wa Azimio atetea kiti chake

Kenia Wahlen 2022
Wapiga kura wa jimbo la KaijadoPicha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Katika matokeo mengine ya uchaguzi Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi wa Azimio alikihifadhi kiti chake baada ya kumbwaga mgombea wa Kenya Kwanza.  Beatrice Elachi naye amekinyakua kiti cha ubunge cha Dagorreti Kusini.

Aidha kiti cha useneta  kimenyakuliwa na Edwin Sifuna wa Azimio ambaye ni katibu Mkuu wa chama cha ODM baada ya kumbwaga mgombea wa Kenya Kwanza Margaret Wanjiru.

Hata hivyo kiti cha ugavana kimenyakuliwa na Jonson Sakaja ambaye alikuwa anawania kiti hicho kwa bendera ya Kenya Kwanza kwa kumshinda mpizani wake Azimio Polycarp Githae.

Katika jimbo jirani la Kiambu, Muungano wa Kenya Kwanza umevishinda viti 11 vya ubunge na Ugavana kati ya viti 12. Kiti kimoja cha ubunge kimenyakuliwa na mgombea wa kujitegema. Itakumbukuwa kuwa jimbo la Kiambu ni ngome ya siasa ya Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.

Soma zaidi: IEBC yakusanya masanduku ya kura

Tayari Moses Kuria aliyekuwa akiwania kiti cha ugavana kwa mwavuli wa Kenya Kwanza kwenye tiketi ya chama cha Kazi amekubali kushindwa na mwezake wa UDA Kimani Wamatangi. Matokeo mengine katika majimbo jirani ya Nairobi kama vile Kajiado na Machakos yanaonyesha kuwa wagombea wa Azimio wameshinda viti vya ugavana na ubunge. Hata hivyo tamko la IEBC linasubiriwa kurasimisha matokeo hayo.

DW, Nairobi