MigogoroUlaya
Norway: Urusi ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu
27 Oktoba 2025
Matangazo
Kombora hilo lilifyetuliwa kutoka visiwa vya Novaya Zemlya vilivyopo kwenye Bahari ya Aktiki. Moscow imesema jaribio hilo lilifanikiwa kikamilifu na kutaja kuwa kombora hilo lina uwezo wa kuepuka mifumo yote ya ulinzi. Hatua hiyo imekosolewa vikali na rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaka rais Vladimir Putin kumaliza vita vya Ukraine badala ya kujaribu makombora mapya.
Aidha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema anatarajia katika siku chache zijazo kwamba washirika wake wa Magharibi watawasilisha pendekezo la amani ili kukomesha vita vyake na Urusi.