1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Nitahakikisha miili ya mateka wote inarejeshwa

16 Oktoba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema atahakikisha Hamas inairejesha miili ya mateka waliosalia huko Gaza, akisisitiza kuwa mapambano "bado hayajaisha".

https://p.dw.com/p/528GS
Jerusalem 2025 | Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia huko JerusalemPicha: Abir Sultan/AFP

Chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump, Hamas iliikabidhi Israel leo jumla ya miili 30 hivyo kufikia idadi jumla ya  miili 120 ya mateka .

Miili ya mateka 19 bado haijulikani iliko, huku Hamas ikisema itahitaji vifaa maalum vya kufukua magofu huko  Gaza  ili kuipata miili hiyo ya mateka iliyosalia. Kundi la kutetea mateka wa Israel limeitaka serikali ya nchi hiyo kuchelewesha hatua zinazofuata za mpango wa amani iwapo Hamas itashindwa kuirejesha miili hiyo.