1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu kuendelea na vita licha ya shinikizo la kimataifa

Josephat Charo
17 Machi 2024

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa tena miito ya kufikisha mwisho vita Gaza mwanzoni mwa kikao cha baraza la mawaziri la Israel mjini Jerusalem Jumapili (17.03.2024)

https://p.dw.com/p/4dp9m
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, alipokuwa katika kikao cha baraza la mawaziri mjini Tel Aviv 07.01.2024Picha: Ronen Zvulun/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema wanajeshi wake watafanya mashambulizi yaliyopangwa ya ardhini katika mji wa kusini mwa ukanda wa Gaza wa Rafah, na kwamba hakuna shinikizo lolote la kimataifa litakalowazuia kufikia malengo yao yote ya vita.

Netanyahu ameitoa kauli hiyo hii leo wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri, taarifa iliyozusha hofu ya kutokea mauaji makubwa ya raia.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekutana kwa mazungumzo na Mfalme Abdulla II wa Jordan na ametoa wito wa usitishwaji haraka mapigano huko Gaza na kusisitiza kuwa hatua ya Israel kushambulia Rafah, inaweza kutatiza mchakato wa amani katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.

Soma pia: Israel yaendeleza mashambulizi yake Ukanda wa Gaza

Netanyahu amewalaumu washirika wake na kusema wamekuwa wasahaulifu wa mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na Hamas Oktoba 7,2023 na kushangazwa na kuona wako tayari kuipokonya Israel haki yake ya kujilinda.