NAIROBI:Rais Kibaki kuwania urasi tena kupitia chama kipya | Habari za Ulimwengu | DW | 17.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Rais Kibaki kuwania urasi tena kupitia chama kipya

Rais Mwai Kibaki anatangaza kugombea tena wadhifa wa rais kupitia muungano mpya wa Party of National Unity.Kauli hiyo ilitolewa katika sherehe maalum.Muungano huo mpya unajumuisha chama cha KANU japo haijulikani iwapo utakuwa na ushawishi mkubwa.

Uchaguzi mkuu unapangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Hii ni mara ya kwanza kwa rais mteule kukabiliwa na upinzani ulio na ushawishi katika uchaguzi mkuu.

Vyama vya upinzani vilitangazwa wawakilishi wao majuma kadhaa yaliyopita ambapo Raila Odinga wa chama cha ODM anagombea nafasi hiyo huku Kalonzo Musyoka akiwaniwa wadhifa huo kwa tiketi ya ODM-Kenya

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com