1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni apeleka jeshi Ruwenzori

Elizabeth Shoo8 Aprili 2016

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametuma wanajeshi katika eneo la milima ya Ruwenzori linalopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya eneo hilo kushuhudia umwagikaji damu tangu uchaguzi mkuu.

https://p.dw.com/p/1IRqF
Ramani ya milima ya Ruwenzori

[No title]

Katika uchaguzi uliopita watu wa eneo hilo waliupigia kura upinzani. Pamoja na hayo, upinzani umedai kwamba hali ya ukosefu wa usalama inayoonekana huko kwa sasa huenda inafanywa na serikali. Kufahamu mengi zaidi kuhusu hali ilivyo na mtazamo wa wachambuzi wa kisiasa kuhusu vurugu, Saumu MWasimba amezungumza na mzaliwa wa eneo hilo ambaye ni mchambuzi wa kisiasa Akol Amazima.