Msimu mpya waanza Tanzania | Michezo | DW | 13.04.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Msimu mpya waanza Tanzania

Kenya FF-shirikisho la dimba la nchi hiyo huenda likafungiwa tena na FIFA.Schalke lazima itambe kesho dhidi ya Mainz ikitaka ubingwa.

Bremen ilipotamba juzi dhidi ya Alkamaar (4:1)

Bremen ilipotamba juzi dhidi ya Alkamaar (4:1)

Viongozi wa Bundesliga -Schalke 04 leo ni leo na asemae kesho kwao ni muwongo:Stadi wao wa kiungo Fabian Ernst amewaonya kabla kuingia kesho uwanjani kwamba itakuwa ni kufa-kupona ikiwa Schalke itawazwe mabingwa msimu huu.Schalke ilitwaa mara ya mwisho ubingwa 1958 kati ya jumla mara 7 iliotawazwa mabingwa wa Ujerumani na hicho ni kitambo kirefu.Na hii ilikua kabla kuanzishwa kwa Bundesliga 1963 .

Mainz maadui zao jioni hii wanapigana wakati huu nao kufa-kupona ili waepuke kuzamishwa daraja ya pili msimu ujao na wanacheza nyumbani.Lakini ikiwa Schalke inastahiki taji,wengi wanadai,lazima wawike mbele ya timu inayopepesuka kushuka daraja ya pili.Maadui zao Werder Bremen walioko pointi 2 tu nyuma wanawasubiri wateleze tu washike usukani wa Ligi.

Hata Stuttgart iliopo nafasi ya 3 na hata Bayern munich iliopo nafasi ya 4 baada ya kupigwa kumbo nje ya champions League zinanyatia kuvaa taji.Bremen ilitamba juzi katika Kombe la UEFA ilipoirarua Al kamaar kwa mabao 4:1-mawili akitia Miroslav Klose.

Na kesho haitatakla tena mchezo katika mpapurano na Borussia Dortmund.Halkadhalika, Bayern Munich ikiwa tumaini lao pekee msimu huu ni taji la Bundesliga,watajitutumua jumapili mbele ya Bayer Leverkusen, ilioaga pia kombe la UEFA kwa kulazwa na Ousasuna ya Spain.

Stadi wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger yameumia na yamkini hatarejea uwanjani msimu huu.

Wiki hii,klabu za bara ulaya zimepatwa na mkosi na kupakwa hata na aibu,kwani klabu 3 za visiwani Uingereza-Manchester united,Chelsea na Liverpool zimetoroka na tiketi 3 za nusu-finali ya champions League kati ya wiki na kuliachia bara hilo nafasi 1 tu ile ya AC Milan.

Milan kwa msangao wa mashabiki wengi wa Bayern munich ilitamba katika Allianz Arena hapo majuzi na kuondoka na mabao 2 na tiketi ya nusu-finali.Munich, iliomudu suluhu ya mabao 2:2 huko Milan wiki 1 kabla, ilidhani ingetamba nyumbani,lakini wapi.

Wakati katika kombe la champions League ni klabu za Uingereza za premier League zilizotamba, katika kombe la UEFAS-kombe la shirikisho la dimba la Ulaya, zilikua klabu 3 za Spian :Mabingwa watetezi sevilla waliongoza njia walipotoka sare 2:2 na mwishoe ushindi wa 4-3 na Spurs.Espanyol ilichukua tiketi ya pili kwa kumudu suluhu 0:0 na Benfica Lisbon na Osasuna ilikongoa meno Bayer Leverkusen na kutwaa tiketi ya tatu ya klabu za spain katika kombe la UEFA.

Shirikisho la dimba la Kenya lakabiliwa tena na msukosuko na FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni.Sababu ni serikali ya Kenya kutokoma kutia mkono wake katika shughuli za dimba la nchi hiyo.

Katika taarifa FIFA iliolipelekea shirikisho la dimba la Afrika-CAF juzi,mjumbe maalumu wa rais wa FIFA Jerome Champagne alionya kwamba kurejeshwa karibuni Kenya katika dimba la kimataifa kunaweza kukafutwa baada ya serikali ya Kenya kutangaza mipango ya kuunda halmashauri ya mpito kuongoza shughuli za shirikisho la dimba la Kenya KFF.

Utakum,buka kwamba Kenya ilipigwa marufuku oktoba mwaka jana isishiriki katika mashindano ya kimataifa kwa kukiuka mapatano ya kimataifa na kwa mizozo isiokwisha ya shirikisho lake la dimba.

Upande wapili wa mpaka,nchini Tanzania,msimu mpya wa Ligi unaanza jumamosi hii huku mabingwa Young Africans wakiumana na Moro united na mahasimu wao wa jadi simba wakiwa na miadi wakati huu na Prison huko Morogoro.

Ligi hii imegawanywa makundi 3 na Yaoung Africans ambayo inaania bado kombe la klabu bingwa la Afrika, haitakubali kuregeza kamba ili kuepuka ule wembe walionyolewa na Esperence usiwanyoe tena kesho.

 • Tarehe 13.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHcN
 • Tarehe 13.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHcN