Mrengo wa Shoto Hamkani Ufaransa | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.03.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mrengo wa Shoto Hamkani Ufaransa

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ufaransa FN kimezusha maajabu katika chaguzi za mabaraza ya miji zilizogeuka onyo kwa chama tawala cha kisoshialisti na kuwaruhusu wafuasi wa kihafidhina kusonga mbele.

Mwenyekiti wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front National,Marine Le Pen

Mwenyekiti wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front National,Marine Le Pen

Chama cha Front National kinachoongozwa na Marine Le Pen kimefaidika na ile hali kwamba idadi kubwa ya wapiga kura hawakuteremka vituoni, wakichoshwa na kashfa kadhaa zinazokigubika chama cha kihafidhina

Tukio jengine la kustaajabisha ni idadi ndogo ya wapiga kura walioteremka vituoni: asili mia 38.72 ya wapiga kura wameamua kutoteremka vituoni-

Mrengo wa shoto umepata pigo kubwa kupita kiasi katika wakati ambapo rais Francois Hollande amepoteza vibaya sana umashuhuri wake,miaka miwili tu baada ya kuingia madarakani .

Mijini Perpignan,Avignon,Forbach,Béziers,Fréjus,na Tarascon chama cha siasa kali za mrengo wa kulia FN kinaongoza matokeo ya duru ya kwanza.Na kina nafasi nzuri ya kushinda kwengineko pia baada ya ushindi wa moja kwa moja katika mji wa Hénin-Beaumont katika jimbo la kaskazini la Pas de Calais ambako Steeve Briois amekipatia ushindi chama hicho kwa mara ya kwanza katika mji wenye wakaazi zaidi ya elfu kumi.

Washoshialisti wajiweke matumaini Paris

Frankreich Kommunalwahlen Paris Nathalie Kosciusko-Morizet und Anne Hidalgo Kombo

Wagombea wawili wa nafasi ya meya wa jiji la Paris(kushoto) Nathalie Kosciusko-Morizet wa chama cha kihafidhina cha UMP na (kulia) Anne HIdalgo Kombo wa chama cha kisoshialisti-.PS

Mjini Paris mgombea wa chama cha UMP Nathalie Kosciusko-Morizet anaongoza mbele ya mgombea wa chama cha kisoshiaalisti Anne Hidalgo.Hata hivyo mrithi wa meya aliyemaliza mhula wake Bertrand Delanoe anapewa nafasi nzur ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi itakapoitishwa jumapili ijayo.

"Hatukutarajia" amesifu M arine Le Pen aliyeutaja uchaguzi huo kuwa wa aina pekee na uliomaliza enzi za vyama viwili vya kisiasa.

Kwa mujibu wa matokeo ya muda yaliyotangazwa usiku wa manane wa kuamkia leo na waziri wa mambo ya ndani Manuel Valls,mrego wa kulia umejikingia asili mia 46,54,mrengo wa shoto asili mia 37.74,siasa kali za mrego wa kulia 4.65 na siasa kali za mrengo wa shoto asili mia0.58.

Serikali huenda ikabadilishwa

EU Gipfel in Brüssel

Rais wa Ufaransa Francois Hollande

Wapiga kura milioni 45 wa Ufaransa na wale wa nchi za Umoja wa ulaya waliakiwa wakatoe sauti zao wakati wa uchaguzi huo ambao unaangaliwa kama kipimo cha umashuhuri wa rais Francois Hollande tangu alipochaguliwa mwezi Mai mwaka 2012.

Rais Francois Hollande huenda akalifanyia mageuzi baraza la mawaziri."Hali inatisha" amesema msemaji wa serikali Nadjat Vallaud Belkacem.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com