1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto wauwa 27 Istanbul

2 Aprili 2024

Watu 27 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa mjini Istanbul, Uturuki, baada ya kutokea moto mkubwa katika jengo moja lililokuwa linakarabatiwa.

https://p.dw.com/p/4eMFO
Vifo vya moto Istanbul
Maafisa wa uokozi wakijaribu kuokowa watu kwenye jengo lililounguwa mjini Istanbul, Uturuki.Picha: ISTANBUL FIRE DEPT./EPA

Moto huo ulianzia chini katika jengo hilo la makaazi ya watu lenye ghorofa 16 kwenye sehemu hiyo hutumiwa kama klabu ya usiku. 

Gavana wa jiji hilo, Davut Gul, aliwaambia waandishi wa habari katika eneo la tukio kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea, lakini akasema kuwa inaaminika miongoni mwa waliokufa ni watu waliokuwa wakihusika na kazi za ukarabati.

Soma zaidi: Erdogan aahidi kurekebisha makosa baada ya kushindwa uchaguzi Uturuki

Waziri wa Sheria wa Uturuki, Yilmaz Tunc, amesema wanawashikilia watu watano kwa mahojiano, wakiwemo mameneja wa klabu hiyo na mtu mmoja aliyekuwa akisimamia ukarabati huo.