1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushirikiano wa vyama vya siasa Uganda NRM, DP wazua maswali

21 Julai 2022

Hatua ya chama tawala nchini Uganda NRM na kile kikongwe cha upinzani DP kusaini mkataba wa ushirikiano imeibua maoni mseto miongoni mwa wananchi na wanasiasa.

https://p.dw.com/p/4ETzz
Uganda | Präsident Yoweri Museveni
Picha: Luke Dray/Getty Images

 Wafuatiliaji wa siasa za Uganda wengi wanaamini kuwa hii ni miongoni mwa mikakati ya rais Yoweri Museveni kujiandaa kuchaguliwa tena bila kupata upinzani mkali kwani amefaulu katika kuudhoofisha upinzani. Mwandishi wetu Lubega Emmanuel ametutumia ripoti ifuatayo.

Sambamba na chama cha UPC, chama cha DP ni chama kikongwe cha kisiasa ambacho wafuasi wake wametambulika kupokeza itikadi za chama hicho kwa watoto wao.

Norbert Mao ndiye rais wa kwanza wa chama hicho kuwa mtu asiyetokeajamii ya Baganda na amekuwa akikabiliwa na upinzani mkubwa ndani na nje ya chama chake kuhusiana na mienendo yake ya kuwashutumu wanasiasa wenzake wa upinnzani kila mara.

Kulingana na Mao hatua hii ya kusaini mkataba wa ushurikiano na utawala ambao siku zote ameukosoa inalenga kudhihirisha kuwa upinzani nchini Uganda umeanza kukumbatia siasa zilizokomaa ambapo kuna ushirikiano wa kisiasa kujenga nchi badala ya kuendelea kuchukulia utawala kuwa adui.

Soma pia:Uganda yakanusha kuwashikilia watoto raia wa Kenya

Mao alimwambia rais Museven kwamba hatua hiyo ni muhimu kwa democrasia ya uganda alioitaja inakuwa na ametengeneza historia kwa wazelendo wa taifa hilo la Afrika Mashariki.

"Hii ni hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa mheshimiwa rais sasa una fursa ya kihistoria kuwaleta pamoja wazalendo wote waliosambaa katika vyama mbalimbali vya siasa" Alisema Mao mbele ya rais.

Je huu ni usaliti wa kisiasa?

Akimpongeza kwa kukubali kuwa na ushirikiano kati ya vyama vyao vya siasa, Rais Yoeri Museveni amekariri kwamba yuko tayari kushirikiana na wapinzani wake wote ikiwa hawatangulizi maslahi yao binafsi bali ya taifa.

Ugandan opposition leaders Robert Kyagulanyi and Kizza Besigye
Viongozi wa vyama vya upinzani Robert Kyagulanyi na Kizza BesigyePicha: AFP/Getty Images

Lakini wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa wanautazama mkataba huo kama kielelezo cha azma ya Museveni kudhoofisha upinzani ili kuepusha joto kali la kisiasa wakati wa uchaguzi.

Soma pia:Museveni: Kupunguza ushuru kutavuruga mipango ya serikali

Wafuatiliaji wa siasa za Uganda wanansema kwamba hatua ya rais huyo wa chama cha upinzani kusaini mkataba huo ni kana kwamba amepoteza mwelekeo wa kisiasa na kusaliti harakatiza wapinzani katika democrasia ya Uganda.

Wambede Wamoto ni mtumishi mstaafu wa serikali, ameiambia DW kwamba hatua hiyo anahesabu kama Mao amechimbia kaburi upinzani nchini Uganda ambao umefanya harakati nyingi hadi kufikia hapo.

"Mwelekeo wa Mao ni kama kusema kwamba ametokomeza chama cha DP na kimemezwa na NRM" Alisema.

Mao: Siwezi kusaliti chama changu wala upinzani

Lakini Norbert Mao anasisitiza kuwa yeye hawezi kusaliti chama chake wala upinzani. Anasema kuwa ukweli wa mambo ni kwamba maslahi ya kitaifa yatangulizwe baada ya rais Museveni kudhihirisha kuwa hataki kuwaacha nje wanasiasa wa upinzani katika utawala wake.

Adui wa Museveni ni Museveni mwenyewe - Bobi Wine

"Nataka kuwahakikishia kuwa siwezi kushawishiwa na pesa na kujiunga na utawala nikikiacha chama changu" Aliwahakikishia waganda punde baada ya kusaini makubaliano hayo.

Wanasiasa mbalimbali wa upinzani wamepokea habari za mkataba huo kwa maoni mseto. Baadhi wanaunga mkono hatua  hiyo wakisema kuwa Uganda inafaa kuiga mfano wa Kenya ambapo mahasimu wa kisiasa huweka tofauti zao mbali na kushirikiana.

Hata hivyo baadhi wanansema huo ni mpango mkakati wa rais Museveni katika kutokomeza ama kufifisha harakati za upinzani katika taifa  hilo ambalo limekuwa limekuwa likilalamikiwa kutopkana na kukandamiza upinzani.

Soma pia:Uganda yatishia kuwafukuza wafanyakazi wa afya wanaogoma

Chama kingine kikongwe cha UPC nacho kina makubaliano ya ushirikiano ijapokuwa mkataba wao na NRM haufahamiki waziwazi. Betty  Among ambaye mke wa kiongozi wa chama hicho Jimmy Akena mwanawe mwanzilishi wa UPC Dr. Milton Obote  ni miongoni mwa mawaziri wanaotokea upinzani.