Mjerumani atekwa nyara na familia yake Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 18.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mjerumani atekwa nyara na familia yake Afghanistan

KABUL

Mfanyakazi wa misaada wa Ujerumani na familia yake wametekwa nyara nchini Afghanistan.

Polisi imesema watu wenye silaha walimlazimisha Harald Kleber mwenye umri wa miaka 42 kutoka kwenye gari lake katika jimbo la magharibi la Herat hapo Jumapili usiku.Shirika la misaada la Ujerumani Green Helmets ambalo seremala huyo wa Kijerumani alikuwa akilifanyia kazi hapo zamani limesema mke wake na mtoto wake pia wanashikiliwa mateka.

Kleber amekuwa akiishi nchini Afghanistan tokea mwaka 2003 ambapo amebadili dini na kuwa Muislamu na kufunga ndoa na mwanamke wa Kiafghanistan.

Maafisa wa serikali ya mitaa wa jimbo hilo wamesema wanaamini kutekwa nyara kwao kumetokana na mzozo wa kifamilia na kwamba kundi la Taliban halihusiki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com