1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSyria

Miezi 6 baada ya tetemeko la ardhi huko Syria na Uturuki

8 Agosti 2023

Miezi sita baada ya matetemeko makubwa ya ardhi kuharibu Kusini Mashariki mwa Uturuki, wakazi bado wanakabiliwa na matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira, nyumba na upatikanaji wa maji safi.

https://p.dw.com/p/4UvQ0
Uturuki
Juhudi za uokozi UturukiPicha: Ylenia Gostoli/DW

Mnamo Februari 6 mwaka huu, matetemeko makubwa ya ardhi yaliharibu maeneo ya kusini mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. Takriban watu 60,000 nchini Uturuki walipoteza maisha na wengine 125,000 kujeruhiwa. Miji 13 iliathiriwa na janga hilo, ukiwemo mji wa Atakya katika jimbo la Hatay kusini mashariki mwa Uturuki. Hali katika eneo hilo bado ni ya huzuni, lakini maisha yanaendelea, ingawa watu wengi wamelazimika kuishi kwenye mahema.

Leyla Seker ni mmoja wa watu wengi waliopoteza makazi yao katika matetemeko hayo ya ardhi. Mwanamke huyo wa umri wa miaka 65 anaishi peke yake kwenye hema, kama maelfu ya watu wengine katika eneo hilo. Amejenga hema yake katika eneo alilokuwa akiishi hapo awali, kwenye shamba karibu na watu wengine 10 hivi.

Bado anaomboleza kifo cha mamake na dadake, wote ambao waliuawa wakati wa matetemeko hayo ya ardhi. Seker ameongeza kuwa sio hao tu waliopoteza maisha lakini pia binamu yake aliyefariki pamoja na jamaa wengine 15.

Syria
Waathirika wa janga la tetemeko la ardhi SyriaPicha: Bakr Alkasem/AFP/Getty Images

Majengo muhimu ya kihistoria kama vile Jengo la Bunge la Hatay na msikiti wenye umri wa miaka 1,500 pia yaliporomoka. Seeker anaelezea kuwa jiji hilo sivyo lilivyokuwa.Wengine waokolewa Uturuki baada ya saa 260

Ingawa tetemeko hilo la ardhi lilitokea miezi sita iliyopita, hali ya maisha kwa wakazi wengi wa Hatay bado ni mbaya sana. Zaidi ya yote, watu wengi wana wasiwasi kuhusu ukosefu wa maji safi ya kunywa.

Seker anaeleza kuwa hali imekuwa mbaya mno na hakujakuwa na hata tone la maji katika muda wa miezi sita na kuongeza kuwa baadhi ya watu wana visima vyao wenyewe wanavyovitegemea kwa maji safi lakini wao hawana kitu.

Mfumo wa usambazaji maji katika eneo hilo uliokuwa umeharibika bado haujarekebishwa. Wakazi kwa sasa wana njia mbili za kupata maji, kununua katika maduka ya jumla ama kunywa maji waliyopewa na mashirika ya misaada yanayoungwa mkono na serikali

Rustem Coklu, wa umri wa miaka 48, ni mfanyakazi wa chuma na mtaalamu wa paa za chuma za nyumba. Baada ya matetemeko ya ardhi kupiga, alikuwa nje kazini  kwa muda. Coklu anasema hakupata malipo ya mara moja baada ya matetemeko hayo kwa sababu watu walikuwa na matatizo mengine ya kushughulikia .Tetemeko la ardhi Uturuki-Syria

Takriban miezi miwili iliyopita, alianza tena kufanya kazi. Ameridhishwa na chakula kinachotolewa kama msaada lakini anasema changamoto ni katika masuala ya usafi, wadudu na joto.

Syria
Misaada kwa wahanga wa tetemeko SyriaPicha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Kulingana na idara ya mipango miji huko Hatay, watu 6000 katika eneo hilo wamepoteza makazi. Wengi aidha walihama miji ama wanaishi katika mahema.

Kabla ya matetemeko hayo adrhi, watu milioni 1.6 waliiishi katika jimbo la Hatay. Serikali imetangaza kujenga majengo mapya ya makazi kwa wale walioathirika kutokana na mkasa huo.

Waziri wa mazingira Mehmet Ozhaseki, anasema serikali inalenga kujenga nyumba 255,000 mpya.

Mara tu baada ya janga hilo, watu wengi walilalamika kwamba misaada ilifika katika eneo hilo kwa kuchelewa, jambo ambalo wengi walishuku kuwa lilichochewa na sababu za kisiasa.Erdogan aapa kuijenga upya Uturuki baada ya tetemeko

Watu wengi pia wanaamini kuwa serikali inapaswa kulaumiwa kwa kiasi fulani kutokana na mkasa huo kwasababu maafisa wake hawakuzingatia onyo la wanasayansi na kuchukua hatua zinazofaa kupunguza athari za matetemeko hayo.