1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfuasi wa Chadema aliyekuwa ametoweka amepatikana

9 Mei 2019

https://p.dw.com/p/3IDhM

Mdude Nyagali, mwanaharakati na mfuasi wa chama cha upinzani nchini Tanzania, Chedema amepatikana usiku wa kuamkia leo katika eneo la Inyala, Mbeya vijijini. Kijana huyo alitoweka siku ya Jumamosi jioni wiki iliyopita huko Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, ikidaiwa alitekwa na watu wasiojulikana. Mawakili wa Mdude walikuwa wamewasilisha shauri mahakamani kutaka mamlaka husika ziwajibishwe na kesi hiyo ilikuwa imepangwa kusikiliza hivi leo jijini Dar es Salaam. Josephat Charo amezungumza na wakili Jebra Kambole, mmoja wa mawakili wa Mdude.