Merkel auponda mpango wa SPD | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Merkel auponda mpango wa SPD

Kansela Angela Merkel wa Ujerumanin Jumamosi (25.02.2017) awashutumu washirika wake katika serikali ya mseto kwa kupendekeza marekebisho kwa magaeuzi ya ustawi wa jamii.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumanin Jumamosi (25.02.2017) awashutumu washirika wake katika serikali ya mseto kwa kupendekeza marekebisho kwa magaeuzi ya ustawi wa jamii ambayo yanapongezwa kwa kuchochea mafanikio ya uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni mgombea wa chama cha SPD amempiku Merkel wakati nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi wa Septemba mwaka huu. Chama hicho kwa miaka kadhaa kilikuwa nyuma ya muungano wa wahafidhina wa Merkel katika uchunguzi wa maoni. Lakini kuungwa mkono kwa chama hicho cha sera za wastani mrengo wa kushoto kumeongezeka tokea kilipomteuwa spika wa zamani wa bunge la Ulaya kuwa mgombea wao mwishoni mwa mwezi wa Januari.

Martin Schulz alitaka kuuvutia upande wa sera za mrengo wa kushoto wa chama chake hapo Jumatatu kwa kusema marekebisho yanahitajika kwa mageuzi ya  "Agenda 2020"

ambayo yaliandaliwa na Kansela Gerhard Schroeder wa chama cha SPD lakini ikamghariu wadhifa wake huo na kukigawa chama.

Mageuzi hayo yaliyozinduliwa mwaka 2013 yalisababisha wanachama wengi wa SPD kujitowa na kujiunga na chama cha sera kali za mrengo wa kushoto Die Linke.

Mpango wa mageuzi wasifiwa

Stralsund Angela Merkel auf CDU-Landesvertreterversammlung (picture-alliance/dpa/S. Sauer)

Kansela Angela Merkel akiwa katika jimbo lake la uchaguzi la Stralsund na kiongozi wa wabunge wa CDU Vincent Kokert katika bunge la jimbo la Mecklenburg-Western Pomerania.

Lakini Merkel ameusifu mpango huo wa mageuzi katika kampeni ya uchaguzi kwenye jimbo lake la uchaguzi la Sraklsund kaskazini mwa Ujerumani Jumamosi kwa kusema "Ndio maana nilisema wakati nilipoingia madaraka miaka 11 iliopita kwamba Kansela Schroeder ametowa mchango mkubwa kwa Ujerumani kwa agenda yake hiyo ya 2010.

Amesema wahafidhina wamefanya baadhi ya marekebisho ya mageuzi tokea mwaka 2005 wakati walipounda serikali ya mseto lakini ilishikilia kiini cha mpango huo kwa sababu uliwapatia ajira watu wengi na kiwango cha watu wasiokuwa na kazi kikapunguwa kwa nusu tokea mwaka 2005.

Merkel amesema lakini siku hizi chama cha SPD hakitaki kuutangaza mpango huo kuwa ni wa mafanikio.Amesema Ujerumani inahitaji kuwa na mdahalo kuhusu Agenda 2025 na amekituhumu chama cha SPD kwa kuendelea kuangalia kipindi chake kilichopita na sio mustakbali wake.

Pia amesema ni muhimu kuiandaa Ujerumani kwa mabadiliko makubwa kupitia utandawazi na kutowa wito kwa makampuni yanayotumia fedha kwa ajili ya utafiti yapunguziwe kodi ili kuzishajiisha kampuni ndogo ndogo zifanye utafiti zaidi.

Malipo ya uzeeni yatetewa

SPD-Kanzlerkandidat Martin Schulz (picture alliance/dpa/C. Charisius)

Martin Schultz kiongozi wa chama cha SPD na mgombea ukansela kwa tiketi ya chama hicho.

Katika hotuba yake hapo Jumatatu Schulz alizungumzia juu ya kuwahami wafanyakazi wazee pamoja na kuanzisha vikwazo kwa mikataba ya kazi ya muda na kutetea malipo ya uzeeni.

Waajiri wanasema jambo hilo litaumiza uchumi.

Schulz ameiambia kampuni ya vyombo vya habari Redaktionsnetzwerk Deutchland  (RND) kwamba anataraji  uchaguzi wa Septemba 24 utakuwa wa mchuano mkali.

Schulz amesema zaidi ya asilimia 20 ya wapiga kura huaumuwa siku kumi za mwisho wakati asilimia mbili hadi tatu huamuwa siku ya uchaguzi yenyewe na kwamba matokeo huenda yakategemea asili hiyo mbili au tatu ya siku ya mwisho

Mwandishi : Mohamed Dahman /Reuters

Mhariri : Lilian Mtono

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com