1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

McChrystal na mikakati mipya Afghanistan

Kabogo Grace Patricia22 Aprili 2010

Kamanda huyo wa majeshi ya NATO nchini Afghanistan ameyasema hayo akiwa Ujerumani baada ya kukutana na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/N2bn
Kamanda wa NATO, Afghanistan Stanley A. McChrystal, (shoti) na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg, (kulia).Picha: AP

Kamanda wa jeshi la Marekani na NATO nchini Afghanistan, Jenerali Stanley McChrystal, amesema mikakati mipya nchini humo ni nafasi ya mwisho kwa ajili ya mafanikio ya kuleta usalama. Hayo aliyaeleza wakati akihojiwa na televisheni ya umma ya Ujerumani. Mapema, Jenerali McChrystal alikutana na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg mjini Berlin na kupongeza mchango wa wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan. Aidha alisema Ujerumani ni mshirika muhimu katika kazi inayofanywa nchini Afghanistan.

Naye Waziri zu Guttenberg alishukuru kutambuliwa huko na aliwanutunukia medali za dhahabu za Ujerumani wanajeshi 14 wa Marekani kwa heshima ya msaada waliotoa kwa wanajeshi wa Ujerumani katika mashambulio ya hivi karibuni. Leo Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel anatarajiwa kuliarifu bunge la nchi hiyo juu ya vifo vya wanajeshi saba wa Ujerumani waliouawa katika wiki za hivi karibuni nchini Afghanistan.