1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kuunda serikali nchini Uholanzi yakwama

Saumu Mwasimba
27 Novemba 2023

Mazungumzo ya kuunda serikali nchini Uholanzi yakwama baada ya kujiuzulu kwa aliyepewa jukumu la kuendesha mchakato huo.

https://p.dw.com/p/4ZVJ8
Uholanzi | Mwanasiasa van Strien
Mwanasiasa van Strien Picha: ROBIN UTRECHT/picture alliance

Kiongozi wa chama cha siasa kali cha Freedom kinacho chukia wageni na Waislamu na kuupinga Umoja wa Ulaya, Geert Wilders amepata pigo kubwa leo baada ya mshirika wake aliyemteua kusimamia mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto kujiondoa kwenye nafasi hiyo kufuatia tuhuma zinazomuhusisha na udanganyifu.

Hatua ya kujiondoa kwa mwanasiasa Van Strien aliyepewa jukumu la kuanza mazungumzo rasmi ya kuunda serikali baadae leo Jumatatu, imeutumbukiza mchakato huo katika mgogoro mkubwa kabla hata haujaaanza huku mikutano yote iliyokuwa imepangwa kufanyika baadae ikifutwa.

Soma pia:Chama cha siasa kali Uholanzi chajipanga kuunda serikali

Viongozi katika kanda ya Umoja wa Ulaya na kwengineko duniani wanafuatilia kwa karibu kuona ikiwa Wilders na chama chake wanaweza kuunda serikali mpya nchini Uholanzi.