Mazungumzo magumu yamkabili Merkel kuunda serikali | Uchaguzi wa Ujerumani 2017 | DW | 25.09.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ujerumani Yaamua

Mazungumzo magumu yamkabili Merkel kuunda serikali

Kansela Angela Merkel amekiri atakabiliwa na mazungumzo magumu ya kuunda serikali ya mseto baada ya uchaguzi wa Jumapili, ambamo vyama vya kihafidhina limepata matokeo mabaya kabisa katika kipindi cha miaka 12madarakani.

na  changanmoto  kubwa  ni  kwamba  uungwaji  mkono  wa  siasa kali  za  mrengo  wa  kulia  unapata nguvu.

Angela  Merkel  ameondoa  uwezekano  wa  kuunda  serikali  yenye wingi  mdogo  bungeni baada  ya  uchaguzi  wa  Jumapili, lakini alikataa  kusema  iwapo anatarajia  kuunda  serikali  mpya  ifikapo mwishoni  mwa  mwaka  huu.

Bundestagswahl | Elefantenrunde Gruppenbild (picture alliance/dpa/G. Breloer)

"Kikao cha tembo" viongozi wa vyama vilivyopata fursa ya kuingia bungeni wakijadili hali baada ya uchaguzi

"Nina  nia  kwamba  tunapaswa  kupata  serikali  imara  nchini Ujerumani," Merkel amesema  katika  mkutano  maalum  uliooneshwa moja  kwa  moja  katika  televisheni  kuhusiana  na  hali  baada  ya uchaguzi  unaowashirikisha  viongozi  wa  vyama  vilivyopata  nafasi ya  kuingia  bungeni, unaojulikana  kama  "mkutano  wa  tembo".

Badala  yake chama  cha  Merkel  cha  Christian Democratic CDU na  chama  ndungu  cha  jimbo  la  Bavaria  cha  Christian Social Union , CSU wanalazimika  kufanya  majadiliano  upya , kuingia katika  muungano  wa  pande  tatu kufuatia  vyama hivyo vya CDU na CSU kupungukiwa  zaidi  ya  asilimia  8 katika  kura  walizopata.

Hii  itakuwa  na  maana  mazungumzo  ya  kuunda  serikali  ya  mseto na  walinzi  wa  mazingira  chama  cha  Kijani  na  kile kinachopendelea  biashara  cha  Free  Democrats FDP baada  ya mshirika  wake wa  serikali  iliyopita  chama  cha  Social  Democrats SPD  kuporomoka  na  kupata  asilimia  20.7  tu, ikiwa  ni  kiwango cha  chini  kabisa  tangu vita  vikuu  vya  pili  vya  dunia.

Angela Merkel (DW/C. Teixeira)

atika ukumbi wa chama tawala cha CDU mjini Berlin wakati kansela alipozungumza na wafuasi wa chama hicho

Wapiga kura waliokimbilia  AfD

Lakini  matokeo  ya  uchaguzi  wa  Jumapili  pia  yana  maana vyama  vya  CDU - CSU vitalazimika  kuwarejesha  wapiga  kura wake  ambao  wamehamia  katika  chama  cha  siasa  kali  za mrengo  wa  kulia  cha  Alternative for Germany , chama  mbadala kwa  Ujerumani AfD, kwa  kusikiliza  kero  zao na  wasi  wasi  wao na  kimsingi  kuendesha siasa  safi, kama  alivyosema  Merkel wakati  akiwahutubia  wafuasi  wa  chama  hicho.

"Ni dhahiri  kwamba  tunakabiliwa  na  mtihani  mgumu, chama cha  AfD  kuingia  bungeni. Tutafanya  tathmini  ya  kina kwasababu tunataka  kuwaresha  wapiga  kura  wa AfD kwa kutatua  matatizo  yao na  wakati  mwingine  wasi  wasi  wao , lakini pamoja  na  yote kwa  kutumia  siasa  safi."

Deutschland Bundestagswahl | AfD Wahlparty | Demo (picture-alliance/dpa/K. Nietfeld)

Waandamanaji mjini Berlin (24.09.2017)wakiwa nje ya jengo ambamo wafuasi wa chama cha AfD walikuwa wakisherehekea ushindi

Muungano  wa  vyama  pamoja  na  FDP  na  chama  cha  kijani utakuwa  na  wingi  mdogo  bungeni  wa  viti  382  katika  bunge  la taifa  Bundestag lenye  jumla  ya  wabunge 700. Chama  cha  AfD ambacho  kiliasisiwa  mwaka 2013 , chama  kinachopinga Uislamu, kinachopinga  Umoja  wa  Ulaya  na  chenye  shaka  kuhusiana  na mabadiliko  ya  tabia  nchi, chama  hicho  sasa  kimejitokeza  kuwa changamoto  kuu  inayoikabili  Ujerumani  baada  ya  vita , kikiwa  na wabunge  zaidi  ya  90 baada  ya  kupata  asilimia  13  ya  kura.

Deutschland Bundestagswahl | AfD Wahlparty | Bystron und Otten (picture alliance/dpa/M. Balk)

Petr Bystron mwenyekiti wa chama cha AfD Bayern (kushoto) na mbunge wa chama hicho Gerold Otten

Kiongozi  wa  chama  cha  kijani Katrin Goring-Eckardt  ameonya kwamba  mazungumzo  ya  kuunda  serikali  mpya  inayojulikana kama  Jamaica  kutokana  na  rangi  za  vyama  hivyo  kufanana  na bendera  ya  Jamaica, ikiongozwa  na  Merkel  yatakuwa  magumu. "Sisi  sio  washirika rahisi,"  amewaambia  waungaji  mkono  wa chama  hicho. Lakini  Merkel  atahitaji  washirika  kuunda  serikali.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Zainab Aziz

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com