Mawaziri wa afya wa G7 wakutana Uingereza | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.06.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mawaziri wa afya wa G7 wakutana Uingereza

Mawaziri wa Afya wa kundi la mataifa tajiri la G7 wanakutana Alhamisi mjini Oxford kujadili njia za kugawana chanjo na nchi masikini.

Waziri wa afya wa Uingereza Matt Hancock atawapokea mawaziri wenzake kutoka Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia na Marekani katika mkutano huo wa ana kwa ana ambapo masuala yanayotarajiwa kuzungumziwa yanajumuisha juhudi za pamoja za kujilinda dhidi ya majanga katika siku zijazo.

Wakati wa mkutano huo wa siku moja, mawaziri hao watajadili pia mkakati mpya wa ulimwengu wa kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Wizara ya afya nchini Uingereza imesema kuwa watakubaliana kuhusu njia mpya ya kimataifa ya kuzuia kuenea kwa magonjwa kwakuwa humusi tatu ya maambukizo yote hutokea kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Kabla ya kuanza kwa kikao hicho hancock alitakiwa na wanahabari kueleza ajenda ya leo na iwapo huu ndio wakati mwafaka wa kutafuta chanjo kwa mataifa yanayoendelea . Hancock alisema kuwa ni muhimu sana na kwamba wanakuja pamoja kutafuta namba wanavyoweza kujitoa katika janag la corona kote duniani.

Großbritannien Coronavirus Matt Hancock

Matt Hancock- Waziri wa afya wa Uingereza

Ameongeza kuwa ni wazi wamepiga hatua kama Uingereza lakini ufanisi utapatikana wakati duniani nzima itakapofanikiwa kukabiliana na janga hilo.
Jumatano, Hancock alisema kuwa zaidi ya dozi nusu bilioni za chanjo ya Oxford/AstraZeneca zimetolewa kusambazwa kote duniani hasa katika mataifa ya uchumi wa wastani na mataifa maskini lakini akatoa wito kwa mataifa tajiri kutoa chanjo zaidi.

Wito wa kamishna wa afya wa EU

Kamishna wa Afya wa Umoja wa Ulaya Stella Kyriakides amehimiza utumiaji wa kasi ya kisiasa katika kuimarisha mifumo ya afya duniani. Kyriakides ameongeza kuwa hakuna wakati wa kupoteza na kwamba kinachohitajika ni ushirikiano thabiti wa ufuatiliaji hasa katika kubadilishana data za vimelea vya magonjwa, na kuongeza kuwa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu zaidi kwasasa.

Mkutano huo unafanyika wakati shinikizo linaongezeka kwa mataifa tajiri duniani kutoa msaada zaidi wa chanjo za Covid-19 kwa nchi masikini ambazo hazina dozi za kutosha kwa mipango kamili ya chanjo. Serikali ya Uingereza imechapisha ripoti mpya juu ya maendeleo ya G7 tangu mwaka 2015 katika kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata chanjo na kudhibiti kuenea kwa maambukizo.

Mkutano huo wa mawaziri wa afya utafuatiwa na ule wa mawaziri wa fedha wa kundi la G7 utakaofanyia kesho Ijumaa ambapo mkuu wa shirika la fedha la kimataifa, IMF , Kristalina Georgieva atawasilisha mpango nafuu wa kumaliza janga la corona kwa kuongeza upatikanaji wa chanjo duniani.