1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa kujadili kuachana na nishati za visukuku

24 Aprili 2026

Mawaziri kutoka karibu mataifa 50 duniani wanakutana nchini Colombia kuanzia leo kwa mkutano wa mazingira utakaojadili mbinu za ulimwengu kuachana kikamilifu na nishati zinazoharibu mazingira ikiwemo gesi na mafuta.

https://p.dw.com/p/5Cl44
Ufuaji umeme kwa njia ya upepo
Nishati jadidifu kama upepo zinapigiwa debe kuwa mbadala wa mafuta, gesi na makaa ya mawe.Picha: Xu Suhui/Xinhua/picture alliance

Mkutano huo wa siku tano ulioandaliwa na Colombia pamoja na Uholanzi utawajumuisha pia wanazuoni na asasi za kiraia kutoka mataifa ya Ulaya, Amerika ya Kusini, Afrika na Asia. 

Marekani na Saudi Arabia miongoni mwa nchi zinazozalisha kwa wingi mafuta hazijatuma wawakilishi hali inayoashiria mgawanyikao katika juhudi za ulimwengu za kuzipa kisogo nishati za visukuku. 

Tofauti na mikutano rasmi ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, mkutano huo wa Colombia hautazamiwi kutoka na maazimio yoyote yenye nguvu kisheria.

Hata hivyo waandaji wamesema mashauriano hayo ni muhimu hasa katika wakati kuna mkwamo wa namna ya kushughulikia ahadi za kuachana na matumizi ya nishati chafuzi kwa mazingira.