Martin Lel ashinda London marathon | Michezo | DW | 14.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Martin Lel ashinda London marathon

Mkenya Martin Lel atoroka na taji lake la 3 la london marathon. Mwenge wa Olimpik waondoka Dar kwenda Oman.

default

Luca Toni aendelea kutamba.

Mwenge wa Olimpik umepita salama-usalimini mjini Dar-es-salaam jana ukielekea sasa Oman.Mkenya Martin Lel ashinda tena London marathon na Bayern munich yairarua Borussia Dortmund kwa mabao 5-0.

Macho ya walimwengu yalikodolewa jana mjini Dar-es-salaam,Tanzania kujionea iwapo visa vilivyopita London,Paris na San Francisco pale mwenge wa Olimpik ulipopita, vingetokea Tanzania.

Wale waliotazamia hayo walivunjwa moyo,kwani mwenge ulipokewa kwa shangwe na shamra-shamra na watanzania huku umati ukijipanga majiani kuulahki kama vile mwanamichezo wetu mjini Dar-es-salaam, George Njogopa anavyosimulia:

London marathon ilimalizika jana kwa ushindi wa Martin Lel kutoka Kenya na huo ukawa ushindi wake 3 baada ya ule wa 2005 na mwaka jana.katika ushindi wake huo, Lel amewseka rekodi ya London marathon ya muda wa masaa 2:05:15 sek. rasha rasha ziliharibu nafasi ya kuwekwa rekodi ya dunia,lakini wanariadha 3 wote walikimbia chini ya masaa 2:06 na pia ni mara ya kwanza mnamo miaka 4 na nusu mwanariadha mwengine mbali na muethiopia Haile Gebreselassie amekimbia chini ya muda huo.Rekodi ya dunia anayo Gebreselassie alioiweka mwaka jana mjini Berlin kwa muda wa masaa 2:4:26 akivunja rekodi ya hapo kabla katika jiji hilo hilo la berlin ya mkenya Paul Tergat.

Sammy Wanjiru pia kutoka Kenya alimaliza wapili akimuachia nafasi ya tatu Abderrahim Goumri.

Katika upande wa wana

Katika Medani ya dimba:Taifa Stars ya tanzania ililipiza kisasi chake kwa Harambee Stars, mwishoni mwa wiki ilipopoitandika mabao 2:0. Wiki iliopita, Harambee stars ilitamba nyumbani Nairobi na kocha wa Taifa stars-mbrazil Maximo akaonya wakenya "kutangulia si kufika".

►◄

Ligi mashuhuri za Ulaya zilikuwa uwanjani na katika Bundesliga,viongozi wa ligi-Bayern Munich waliendelea kutanua mwanya wao kileleni hadi pointi 9 na hakuna tena wasi wasi kwamba taji msimu huu ni lao.

Munich jana ilivuma kwa kishindo ilipoirarua Borussia Dortmund kwa mabao 5-0.Pigo hilo liliiabisha Borussia Dortmund machoni mwa mashabiki wake na hata kocha wake.

Meneja wa Bayern munich, Uli Höness akiuelezea ushindi wa klabu yake jana alisema:

"Kile ambacho timu yetu imeonesha nusu saa ya kwanza ya mchezo ilikua dimba la kumpendeza mtu kabisa ,lilikua dimba kutoka sayari nyengine ,kwani kila bao liliandaliwa maridadi ajabu na lilistahiki malipo ya kiingilio uwanjani."

Nae kocha wqa Borussia Dortmund, Thomas Doll alisema:

"Naomba radhi kwa mashabiki wote wa B.Dortmund kwa jinsi tilivocheza leo,kwani kilichofanyika leo ni sawa na kutiwa kitanzi.Nisingependa kuona tena timu yangu ikifedheheshwa namna hii."

Bayern munich sasa ina pointi 60 huku mapambano 6 tu yakisalia kukamilisha msimu.Schalke imemtimua kocha wake Mirko Slomka baada ya kuzabwa mabao 5-1 na Werder Bremen ambayo sasa inakamata nafasi ya pili ikiwa pointi 2 zaidi kuliko Schalke.

katika Premier League-ligi ya Uingereza, Manchester united inaendelea kutamba na kama Bayern munich ,Ujerumani, MANU ina nafasi nzuri ya kubakia na taji.Manchester iliilaza Arsenal mabao 2-1 na kuvunja ubishi wao.

Chelsea wako pointi 6 nyuma na hata wakiishinda leo Wigan ,hawaifikii Manu.

Katika La Liga-ligi ya Spian Real madrid imepiga nayo hatua moja kulibakisha kombe kabatini mwao.Real iliondoja na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Real murcia.Kwa kushindwa kw Villareal bao 1:0 na Almeira na Barcelona kumdu suluhu ya mabao 2:2 na Huelva.

Nchini Itali, Inter Milan nusra itzeleze mbele ya Fiorentina lakini iliweza mwishoe kuondoka na ushindi wa mabao 2-o.As roma ikiwa nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi inaendelea kuitia shindo Inter Milan kileleni .Iliondoka Roma na ushindi wa bao 1-o dhidi ya udinese.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com