1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano makali yashuhudiwa kusini na kaskazini mwa Gaza

15 Mei 2024

Vikosi vya Israel vimepambana na wanamgambo kwenye Ukanda wa Gaza leo Jumatano, ikiwemo katika mji wa kusini wa Rafah, ambako ni hifadhi ya mamia kwa maelfu ya Wapalestina wanaokimbia mapigano yaliyodumu kwa miezi saba.

https://p.dw.com/p/4ftan
Magari ya kivita ya Israel karibu na Gaza
Magari ya kivita ya Israel yakiwa yamepiga kambi karibu na mpaka wa Ukanda wa GazaPicha: Abis Sultan/EPA

Vikosi vya Israel vimepambana na wanamgambo kwenye Ukanda wa Gaza leo Jumatano, ikiwemo katika mji wa kusini wa Rafah, ambako ni hifadhi ya mamia kwa maelfu ya Wapalestina wanaokimbia mapigano yaliyodumu kwa miezi saba.

Waakazi wa Rafah wamesema vikosi vya Israel vimesogea hadi kwenye vitongoji vitatu vya mji huo huku wapiganaji wa Kipalestina wakijaribu kuwazuia kulifikia eneo la katikati mwa mji.Wapalestina na kumbukumbu ya miaka 76 ya Nakba

Katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, kaskazini mwa Gaza, wakaazi wamesema vifaru vya Israel vimezivunja nyumba kadhaa lakini wanajeshi wake wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa Hamas na kundi la Islamic Jihad.

Mapambano hayo yameshuhudiwa katika siku ambayo kumefanyika kumbukumbu ya miaka 76 ya siku ya Nakba inayokumbuka masaibu ya mamia kwa maelfu ya Wapalestina waliolazimishwa 

kuihama ardhi yao katika mapigano yaliyofungua njia ya kuundwa kwa taifa la Israel mnamo mwaka 1948.