1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yaahirisha mara ya saba kesi ya mwandishi habari

7 Novemba 2019

Mahakama nchini Tanzania imeahirisha mara 7 kusikilizwa kesi ya mwandishi habari maarufu aliyekamatwa Julai mwaka huu katika kesi ambayo mawakili wake wanasema inashawishiwa kisiasa.

https://p.dw.com/p/3Sc7O
Tansania Erick Kabendera vor Gericht
Picha: DW/S. Khamis

Erick Kabendera, mwandishi  habari  mwenye  makao  yake mjini  Dar es Salaam ambaye amekuwa  akiripoti  katika majarida  ya  kimataifa, ameshitakiwa  mwezi  Agosti  kwa uhalifu wa  kupangilia, kukwepa  kulipa kodi na  utakatishaji fedha.

Jaji katika  mahakama  ya  Kisutu mjini Dar es Salaam ameahirisha  kesi  hiyo  hadi Novemba 20.

Kama  kesi  nyingine  tangu mwezi Agosti, mwendesha mashitaka  ameiambia  mahakama  kuwa  uchunguzi  bado haujakamilika, wakati  mawakili  wa  Kabendera  wametaka kesi  hiyo  iendelee  kutokana  na hoja kwamba  mteja  wao anashikiliwa kwa  mashitaka  ambayo  hayana dhamana.

Jaji anayeshughulikia kesi  hiyo amepandishwa  cheo kwenda  katika  mahakama nyingine  na  jaji  mpya hajakabidhiwa  kesi  hiyo. Mawakili wake na kundi la wanaharakati wa haki za binadamu wanadai kesi hiyo inashawishiwa kisiasa.