1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yasababisha uharibifu mkubwa huko Gaza

19 Novemba 2025

Raia wa Gaza wanakabiliwa na hali ngumu baada ya mvua kubwa za hivi majuzi zilizosababisha mafuriko na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu muhimu.

https://p.dw.com/p/53ti6
Gaza 2025 | Wapalestina wakijaribu kurekebisha mahema yao baada ya mafuriko
Wapalestina wakijaribu kurekebisha mahema yao baada ya mafuriko yaliyosababisha uharibifu mkubwaPicha: Khames Alrefi/Anadolu Agency/IMAGO

Vitu kadhaa kama mahema, magodoro, mablanketi, chakula na dawa vimesombwa na maji kufuatia mafuriko hayo. Mamlaka ya Gaza inayoongozwa na Hamas imesema hasara iliyotokana na mafuriko hayo inakadiriwa kufikia dola milioni 4.5 za kimarekani, na kwamba mahema 22,000 yameharibiwa.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa hali ni mbaya mno huko Gaza. Aidha, mashirika ya misaada ndani ya  Gaza  yamesema mahema mapya yapatayo 300,000 yanahitajika haraka ili kuwasaidia Wapalestina ambao idadi kubwa hawana makazi kufuatia uharibifu mkubwa uliosababishwa na vita.