Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia milioni 1 Afrika | Matukio ya Afrika | DW | 07.08.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia milioni 1 Afrika

Zaidi ya watu milioni moja wameambukizwa virusi vya Corona barani Afrika.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP, ni kuwa bara hilo limerekodi maambukizi 1,000,054 huku kiasi ya watu 21,724 wakifariki kutokana na ugonjwa huo wa Covid-19.

Idadi ya maambukizi hayo ni asilimia tano tu ya maambukizi yaliyorekodiwa duniani kote.

Vilevile, idadi ya maambukizi huenda ikaongezeka kutokana na hofu ya kutokea kwa wimbi la pili la mlipuko wa virusi vya Corona licha ya baadhi ya mataifa kuonekana kufikia kilele cha maambukizi.

Kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika ACDC, ni kuwa nchi tano barani Afrika zimerekodi asilimia 75 ya maambukizi kote barani humo.