LUSAKA: Wazimbabwe wahifadhi amani na utulivu | Habari za Ulimwengu | DW | 17.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA: Wazimbabwe wahifadhi amani na utulivu

Rais Levy Mwanawasa wa Zambia ametoa mwito kwa Wazimbabwe kuhifadhi amani na utulivu.Mwanawasa alikuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa jumuiya ya ushirikiano na maendeleo ya kusini mwa Afrika,SADC.

Alisema,nchi zote za kanda hiyo zimepitia wakati mgumu,lakini hazijatumia nguvu.Matatizo ya kisiasa na kiuchumi katika nchi jirani Zimbabwe, ni mada kuu katika mkutano huo wa kilele mjini Lusaka.

Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini anaongoza juhudi za upatanisho kati ya Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na wapinzani wake wa kisiasa.Maafisa wa chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe MDC wamesema,juhudi za upatanisho za Rais Mbeki zinachukua muda mrefu mno.Naibu rais wa MDC,Thokozani Khupe amesema,SADC yapaswa kuchukua hatua kwa haraka,ili kuzuia maafa makubwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com